Menu
 


Hitmaker wa Mpenzi Jini, Binti Kiziwi, na nyinginezo Z ANTO amesema hakuna msanii mzuri ambae anamuumiza kichwa wala hakuna msanii ambae anaimba vizuri kwa sasa na kufanya kitu cha ajabu ambacho kitamuogopesha.

Akipiga stori na chumba cha sindano cha KALI ZA BOMBA YA BOMBA FM "wasanii kwa sasa wengi wanakosa ubunifu na kupelekea kubebwa na promotion, ni ndoto kwa wasanii wa kibongo kuchukua tuzo za Afrika kama kora kwa sababu wasanii wengi wamekuwa wanacopy staili za wasanii kutoka nje ya nchi".
 Bofya hapa kumsikiliza.


Aidha amezungumzia ukimya wake katika gemu kwa sasa unasababishwa na maujukumu yake ya kimaisha ambapo kwa sasa anajipanga kurudi kurudi upya na kuhakikisha muziki wa bongo unatambulika na staili yake.

Post a Comment

 
Top