Bonge la Nyau(Kulia) na Bob Junior(Kushoto).
Hitmaker wa Wengi Walaghai LAMECK PHILIPO a.k.a BONGE
LA NYAU mwezi huu anatimiza mwaka mmoja toka kuingia kwake katika gemu la
muziki na ameeleza kupata mafanikio
mengi baada ya kuwepo kwenye KILI MUSIC
AWARDS 2013 iliyofanyika June mwaka huu na vilevile kumwezesha kupata show
nje ya nchi.
Akipiga Stori na kipengele cha Chumba Cha Sindano kupitia
kipindi cha Kali za Bomba hapa Bomba FM Mbeya, Msanii BONGE LA NYAU ameeza kuwa kwa sasa ana kila sababu ya kujivunia
mafanikio aliyoyapata mpaka sasa.
“Namshukuru Mungu kwa
sababu nimeanza muziki mpaka leo huu mwezi natimiza mwaka tangu nimeanza kutoa
nyimbo Official, kwa hiyo nyimbo yangu ya kwanza ilikuwa Wengi walaghai ile nashukuru Mungu, nyie
mapresenter, Media zote zilinisapoti vizuri
watu wakaipokea nikaweza kuingia hadi kwenye tuzo ikanifanya watu wengi
wanijue, watu wengi wanipe credit nikapata mialiko sehemu mbalimbali Mombasa,
yaani nimefanya show sehemu nyingi kupitia ile nyimbo kwa mapokezi yake ni
mazuri pia baada ya hapo nikatoa nyimbo yangu ya Gusa Unase nayo ikapokelewa
vizuri japo sijaachia audio nilitoa video tu pia watu wameipokea vizuri”
alisema BONGE LA NYAU.
Kwa hatua nyingine BONGE
LA NYAU amemshukuru Mtayarishaji wake wa muziki(Producer) BOB JUNIOR kwa kumfunza kufanya
miondoko tofauti tofauti ya muziki ili kuendana na soko na ushindani wa sasa
“Off cause credit za kwanza namshukuru sana Producer wangu mimi nilikuwa
sifanyi miziki hiyo unajua mimi napenda sana ku-rap, na-rap sana lakini
producer wangu BOB JUNIOR ambaye
alikuwa ananikomalia lazima tufanye kitu ambacho kitatuingizia pesa, tusifanye
muziki ambao tutafanya tu watu watafeel lakini hautopigiwa simu kualikwa
kufanya show”.
BOFYA HAPO CHINI KUSIKILIZA MAHOJIANO ZAIDI:-
Post a Comment
Post a Comment