Menu
 Hitmaker wa Tushukuru kwa Yote DITTO amesema sababu zinazomfanya afanye innovation  ya nyimbo za zamani zilipendwa ni kuwafanya wadau wa muziki kuzikumbuka na kuzisikiliza kutokana na kuwa na ujumbe wenye mafunzo  ya kimaadili ndani ya jamii.

Akipinga Stori na Chumba Cha Sindano kupitia kipindi cha Kali za Bomba cha kituo cha redio Bomba FM Mbeya hapa DITTO anaeleza “Kutoa wimbo au kutoa wimbo ni kutokana na Plan ambazo mimi mwenyewe niko nazo ndio zinazonilazimisha nifanye muziki wa aina gani, nirekodi nyimbo gani ndio huko sasa  unatuta tuko katika kufanya nyimbo za kizamani kitu kizuri unajua kwamba ni nini nikurudisha zile nyimbo zilifanya vizuri sana katika kipindi chao, sasa ni lazima pia nyimbo ziendelee kuwepo sisi tunafanya kurudia maana ya kuzirudia nikufanya yaani kitu ambacho watu watakuwa wanakumbuka zile ambazo zilikuwepo, samahani innovation wanaita unaendelea kuifanya iwe na thamani ile bidhaa iliyokuwepo katika kipindi cha nyuma”.

DITTO alipoulizwa sababu za kufanya innovation ikiwa wasanii wengi wakifanya muziki wa kuchezeka kwa kunakili muziki wa kimagharibi na hapa anajibu “Unajua kila mtu ana mikakati yake ana malengo katika kitu ambacho yeye anaingia sasa mimi malengo yangu kuingia katika muziki kwanza nikuhakikisha mtu ambaye nakuwa mtu ambaye tayari na utambulisho wangu wa aina ya muziki ambao naufanya yaani kwamba ukiusikia unajua aaah! DITTO huyo, sifanani na mtu yeyote ukisikiliza muziki wangu uko tofauti jamaa anaimba anaandika vizuri na hayo ndio malengo yangu, ushanifahamu sasa kuna mwingine  anaweza akawa na plan labda ya kutoka afanane na mtu fulani  au atoke afanane na kitu fulani. Ushauri wangu katika jambo kama hilo kila mtu atembee katika malengo yake”.

Hata hivyo DITTO ameeleza sababu za kuchelewa kuachia nyimbo katika vituo vya redio na televisheni alikuwa na haya ya kusema “Ukimya huu mambo yanaenda ipo kampuni inaitwa GREEN LIGHT MUSIC AND COMPANY mimi ndio ambaye naiendesha lakini Share holder  ni AMINI tumekuwa tunajishughulisha na masuala mengi ya uandishi wa nyimbo, Ku-Create kampeni tofauti za makampuni mengine mengine, Ringtones, Vipindi vya TV na yaani mambo mengi ambayo tumekuwa tunayafanya lakini asilimia nyingi pia matangazo kwa sababu napiga katika redio ujue sisi ndio tunayafanya kwa hiyo watu wasione ukimya kuna shughuli nyingine naendelea nazo huku chini naifanya nyingi tu bado naendelea kuzitumia veriety za muziki katika kufanya shughuli nyingine”.
BOFYA HAPA KUSIKILIZA. 
 

Post a Comment

 
Top