Menu
 

Na Mwansishi wetu. Jaji Mkuu wa Tanzania Mheshimiwa Mohamed Chande Othman ameeleza kuwa kuanza kutekelezwa kwa sheria ya adhabu mbadala kutaondoa hali ya sasa ya msongamano wa wafungwa katika magereza nchini pamoja na kupunguza matumizi ya fedha za kuhudumia wafungwa.

Jaji Mkuu amesema hayo leo jijini Dar es salaam alipokuwa akizungumza katika ufunguzi wa mkutano wa nchi za afrika unaohusiana na matumizi ya sheria mbadala katika utekelezaji wa hukumu zinazotolewa na mahakama katika nchi hizo.

Jaji mkuu ameeleza kuwa kwa sasa hali ya mrundikano wa wafungwa katika magereza hapa nchini  imekuwa ikiongezeka na kuchangiwa na kuwapo kwa idadi kubwa ya wafungwa ambao kama wangehukumiwa kutumikia vifungo vyao kupitia sheria ya adhabu mbadala ya mwaka 2002 ongezeko hilo lingepungua.

Naye mwenyekiti wa taifa wa kamati ya huduma za jamii Jaji Shabani lila ameeleza kuwa ufinyu wa bajeti,vitendea kazi na uhaba wa watumishi hususani maafisa ustawi wa jamii nchini kumekuwa ni kikwazo kwa utekelezaji wa sheria hiyo.

Jaji LILA ameeleza kuwa mpaka sasa sheria hiyo imeanza kutekelezwa katika mikoa 17 na katika wilaya 35 za Tanzania bara.

Post a Comment

 
Top