Menu
 


Katika maisha ya mwanadamu hakuna mtu ambaye anaishi bila kujiwekea malengo yake kuwa nani hapo baadae kadiri muda, siku, wiki, miezi na miaka inavyosonga mbele, kama ilivyo kuwa kwa Hitmaker wa Mama Mubaya MATALUMA ambaye malengo yake yalikuwa ni kuwa Fundi Makenika na si kuwa mwanamuziki.Akipiga Stori na kipengele cha Chumba Cha Sindano kupitia kipindi cha Kali za Bomba cha kituo cha redio Bomba FM cha jijini Mbeya  MATALUMA “Mimi ujue kazi kubwa ni muziki nimesomea ufundi Makenika na sasa shule yenyewe sikumaliza kwa hiyo nikakosa cheti, hilo lilikuwa lengo langu kubwa sio kuimba, lakini ilitokea ghafla ninaimba na ninaweza na  watu wakanishauri  kuwa naweza nikapelekwa THT, ma THT ni sehemu ambayo haina na mkataba kusema kwamba unasaini kwamba wewe ni mtu wao unafanya kazi unakuta umeshatoka, umehit kwa hiyo wewe mwenyewe roho yako inakutuma niendelee nisiendelee, niwepo  nisiwepo”.Hata hivyo alipoulizwa MATALUMA kama mkataba hauwepo labda ni dhana gani mbadala hujengewe msanii ili kujiendeleza? “Alikuwa na haya ya kusema “Haikuambii chochote kuwa itakusaidia hiki au nini hiyo haipo, kwa hiyo kwa vitu kama hivyo kwa vitu kama hivyo unakuta changamoto mzigo mkubwa inabidi niubebe mimi mwenyewe kama mimi mwenyewe, inakuwa kazi ngumu kama sina menejimenti ambayo inakuwa inajali labda imeandika katika mikataba kwamba tutakusaidia hiki, tutakusaidia hiki kidogo inakuwa inakupungumzia matatizo”.
BOFYA HAPA KUMSIKILIZA. 

Post a Comment

 
Top