Menu
 


Hitmaker wa Nichuum RAHEEM RAMADHAN a.k.a BOB JUNIOR amesema kiasi cha pesa Dola elfu 10 za kimarekani, sawa na zaidi ya shilingi Milioni 15 za kitanzania kitatumika kukamilisha video ya track yake ya BASHASHA aliyomshirikisha VANESSA MDEE itakayofanywa na kampuni ya OGOPA VIDEOS kutoka nchini Kenya.


Akipiga stori na Chumba Cha Sindano kupitia Kipindi cha Kali za Bomba cha Kituo cha redio Bomba FM Mbeya, BOB JUNIOR ameeleza pia ngoma yake ya Bashasha imepokelewa vizuri kuliko ngoma zake zote toka kuanza kwake muziki.“Safari hii miguu ya shingo tu kwa kila mtu, Video tuna-shoot jumatano inayofuata yah!, lakini ni nyimbo ambayo kwakweli toka nimeanza muziki hii ni nyimbo ambayo umepokelewa kwa nguvu sana sijawahi kuona. Mazingira ya video ni mazingira ni makubwa kwa kweli tumeandaa Dola elfu 10, kwa ajili ya video ya bajeti hiyo sijui sasa kama itamalizika, itaisha lakini bajeti ipo tu imewekwa milioni 16 ya kibongo”.Kwa hatua nyingine BOB JUNIOR ameeleza harakati za kukamilisha video hiyo huku akisisitiza kuwa ubunifu na vitu vya tofauti zaidi vinategemewa kung’arisha video hiyo ili kuleta ushindani zaidi “So sijui wenyewe wanachotaka kukifanya ila kuna vitu ambavyo tumeambiwa tuvitimize, location na kila kitu ambavyo siwezi kutaja kwa sasa, lakini update nyingi utapata kwenye mablogs, kwenye mainternet, kwenye whatsApp ukitaka nikutumie picha kipindi ambacho tutakaribia kushoot, kwa sasa siwezi kutoa opinion yoyote kwa tutashoot wapi wapi au wapi wapi kwa sababu kila kukicha najaribu kuongeza idea hii video ifanyike vipi”.
BOFYA HAPA CHINI KUMSIKILIZA ZAIDI BOB JUNIOR.
 

Post a Comment

 
Top