Menu
 


Hitmaker wa Dear God, KALA JEREMIAH amesema Serikali inapaswa kuboresha miundombinu ya kufundishia, na malipo ya mshahara yenye uwiano sawa na kazi ngumu inayofanywa na Walimu sambamba na kuboresha Mitahala ya elimu itakayowawezesha wanafunzi kufanya vema katika mitihani yao.

Akipiga stori na Kipengele cha Chumba Cha Sindano kupitia kipindi Kali za Bomba cha Kituo cha redio Bomba FM 104.0MHz Mbeya rapper KALA JEREMIAH anasema “Mimi kwanza naona matatizo yako katika sehemu mbili. Tatizo la kwanza lipo kwenye mitahala kufeli na kufaulu kunategemeana na Mitahala, lakini tatizo la pili ni walimu, uwezeshwaji wa walimu, tuna walimu wazuri lakini hawana malipo mazuri kwa hiyo wanakuwa wanajikuta wanafanya mambo mawili kwa wakati mmoja wanashindwa ku-concentrate kwa kile ambacho walitakiwa kukifanya kwa hiyo kwa mimi naona matatizo mawili makubwa sana ya msingi sana mishahara ya walimu na uvovu wa  mitahala”.

Hapa anazungumzia mtazamo wake juu ya mabadiliko yaliyokuwa yametangazwa na Wizara ya elimu na mafunzo ya ufundikuhusu viwango vya ufaulu kwa shule za Sekondari hapa nchini kuwa hayana tija kwa maendeleo ya elimu “Kwa hiyo nadhani kubadilisha viwango vya kufaulu sio dawa, yaani vitu vingine dawa  ni kurekebisha sehemu hizo mbili walimu wapate malipo mazuri angalau ambayo yanaendana na kazi wanayoifanya lakini pia  mitahala, mitahala iliyopo ni mitahala iliyoduma yaani wanafundisha kupitia mitahala ya kizamani sana lakini mimi kwa mtazamo wangu naona hivyo. Inaweza kuongeza idadi ya wanafunzi kufaulu haiwezi kuongeza uwezo wa  watu kutambua vitu ndio maana nasema unajua viongozi  wanawasomesha watoto wao nje au kwenye mashule binafsi ambayo ya kimataifa(International School), ambazo wanafundisha kupitia mifumo tofauti sana na mifumo inayofundishwa katika mashule ya kawaida”.

Aidha KALA JEREMIAH hakuishia hapo na hapa anaendelea kusisitiza zaidi. “Kwa hiyo nadhani yaani kikubwa ni hicho kujaribu kuangali kulazimisha vitu hivyo viwili viwe sawa, kulazimisha kuwe mitahala kuwa mizuri jinsi ya kumfundisha mtu, unapomfundisha mtu  ndio anavyoelewa, huwezi ukamfundisha mtu vibaya akaelewa vizuri au ukamfundisha vizuri akakuelewa vibaya na dhani mimi nitaendelea kukomalia hapo”.
HAPA MSIKILIZE ZAIDI .

Post a Comment

 
Top