Menu
 

Wanasema mla ndizi husahau ila mtupa maganda kuweka kumbukumbu zaidi ya ‘memory card’, hii ndiyo imemkuta The Mother Monster ‘Lady Gaga’ ambae mwaka 2009 aliandikiwa wimbo wa ‘Teeth’ na mwandishi maarufu ambae pia ni mwimbaji ‘Riley’ na kuahidi kumlipa 25% lakini baadae akakausha kama amesahau kuwa jamaa alihusika katika wimbo huo.Lady Gaga ashitakiwa kwa kukwepa kumlipa mwandishi wa wimbo wake

Baada ya miaka minne ya kusubiri chake kutoka kwa Lady Gaga bila mafanikio, Riley ameamua kudai haki yake kupitia vyombo vya sheria.
Kwa mujibu wa TMZ, Riley ambae ni mshindi wa tuzo za Grammy amefungua mashitaka akidai malipo ya wimbo huo uliokuwa kwenye album ya ‘The Fame Monster’ kiasi cha dola 500,000 pamoja na fidia ya usumbufu.
Bado Lady Gaga hajasema chochote kuhusu tuhuma hizo na sasa hivi anaendelea kuiweka sawa album yake ‘ARTPOP’ inayotarajiwa kutoka November 11, mwaka huu.

Post a Comment

 
Top