Menu
 


Saynag katika pozi.
Hitmaker wa Inatosha, Nafsi inauma SAYNAG ABRIHHAN a.k.a SAYNAG amesema sababu za ukimya wake katika gemu umetokana na matatizo ya kifamilia baada ya kufiwa na Mama yake mzazi.

Akipiga stori na Chumba Cha Sindano kupitia Kipindi cha Kali za Bomba cha Kituo cha redio Bomba FM Mbeya, SAYNAG ameeleza kuwa “kuna watu wanajua mimi nilifikwa na matatizo na msiba, kuna wengine hawajui hilo suala yaani yote hayo ni kutokana na matatizo ambayo marehemu mama yangu alikuwa nayo. Kwanza alikuwa anaumwa sana kwa hiyo nilikuwa sina muda wa kuingia studio kurekodi, kichwa change chote kilikuwa kina muwaza kwanza mama yangu, nilikuwa nataka apate afueni kwanza halafu niendelee na kazi zangu lakini haikuwa riziki kwa hiyo pia nikazindi kuchanganyikiwa kwamba nimemkosa pamoja na jitihada zangu, sikuwa na muda wa kufikiria kutoa nyimbo kwa wakate ule, sikuwa na muda wa kufikiria show, siku na muda wa kufikiria chochote zaidi ya kile kitu ambacho kilichokuwa kinaniumiza,  lakini hayazoeleki ila kutokana na hali halisi inabidi nikubaliane na hali halisi ilivyo kwa sasa inabidi niendelee tu na kazi zangu, lakini ni mtu aliyekuwa ananipa sapoti kubwa katika kazi zangu”.

Aidha SAYNAG amesema kuna changamoto nyingi ambapo kwa baadhi ya wasanii wenzake wenye menejimenti za uhakika wapo radhi wamzipe mtu Fulani atoke mtu Fulani kwa ushwawishi wa nyimbo kutopata airtime katika vituo vya redio na Tv kwa wasanii wengine wasio na menejimenti.
 “Lakini naamini kama wewe msanii unajua nini unachokifanya unaendelea tu kufanya kama mimi au watu wengine ambao hawasimamiwi au wanajisimamia mwenyewe, Kipaji mimi kama nakipaji  changu najiamini sehemu wowote hata kama mtu ataamua anizibe mimi lakini still wapo wanaokubali na wanataka uwepo kila siku siangalii nani yupo chini nani yupo juu mimi naangalia kazi yangu na mashabiki wanahitaji kitu gani, mara nyingi nilikuwa nasikia sana mashabiki wanalalamika kwenye mainternet kwamba sijatoa nyimbo mbona niko kimya, wanaona kama nimeacha gemu ni kipaji ambacho ninacho mwenyewe yaani, sifosiwi namaanisha sitafuti mtu anitungie, kwa maana kwamba amesusa kunitungia sasa hivi  wimbo, kwa hiyo nimeamua kunyamazwa kwa sababu sinanyimbo ya kutoa hapana, natunga mwenyewe natafuta melody mwenyewe, kwa hiyo ni kitu ambacho ninacho milele siwezi kukiacha kwa hiyo wao wasubirie tu sasa hivi nipo vizuri nitaachia track niliyomshirikisha BEKA sambamba na video niliyofanya na BLUE.
BOFYA HAPA CHINI KUMSIKILIZA ZAIDI SAYNAG.

Post a Comment

 
Top