Menu
 


Hitmaker wa Umekwenda na Nipe Muda NEY LEE  anatarajia kufanya Listening party ya Albamu yake ambayo mpaka sasa hajaipa jina, November 17 mwaka huu akianzia nyumbani kwao Jijini Mbeya akisindikizwa Legentary JUMA NATURE na vilevile ataachia Filamu yake Februari 2014.

Akipiga stori na Kipengele cha Chumba Cha Sindano kupitia kipindi Kali za Bomba cha Kituo cha redio Bomba FM 104.0MHz Mbeya  NEY LEE anasema jina la Albamu hiyo itakuwa ni Surprise hadi siku ya uzinduzi kama anavyofafanua “Okay albamu yangu mpaka sasa hivi sijajua nitaiitwaje, lakini tayari albamu yangu ipo inakuja naanza na Mbeya tarehe 17 nitakuwa Mbeya lakini siwezi kusema ni wapi kwa sababu bado ni mapema na vitu vyote tayari vimesha-arrangejiwa lakisi nafikiri soon nitawajulisha wote itakuwa sehemu gani nitasindikizwa na JUMA NATURE kwa hiyo nikitu ambacho sasa hivi nipo katika mchakato wa kukifanya na ni kitu serious kabisa”.

Akizungumzia zawadi na fursa alizoziandaa kwa mashabiki wake NEY LEE amesema “Kwa hiyo itafanyika Listening party na nita-launch album yangu mwezi wa 12 kwa hiyo watu watasikiliza nyimbo, na watu wataweza kupiga picha na mimi, kuongea na mimi, kuniuliza maswali mengi coz itakuwa friendly show kwa hiyo watu wengi waje waone wasikie kabla ya kununua kile watakacho kinunua wawe wameshakisikia kutoka before, kwa hiyo nimeanza na Mbeya peke yao ambao wataweza kusikia nyimbo zangu kabla ya kununua albamu(kwa msisitizo) ila sehemu nyingine nitauza kawaida tu, sitotaja jina mpaka siku ya show yenyewe”.
 
Hata hivyo NEY LEE akitolewa ufafanuzi idadi ya nyimbo zinazopatikana katika albamu hiyo na wasanii alioshirikiana  nao pamoja na Movie yake ambayo nayo hajaipa jina ameeza kuwa “aaah nyimbo zitakuwa si chini ya nane, kuna collabo kuna nyimbo nilizofanya mimi kama mimi, humo ndani kuna nyimbo nilizofanya na Linex, Kala Jeremiah na Ally Nipishe. Filamu bado tunashoot, unajua filamu sio kitu chepesi kumalizika  bado scene nyingi zinaendelea bado ipo na itatoka na niliahidi kama Mwezi wa Pili mwakani kwa hiyo ila siwezi kutaja jina lake kwa sababu nikitaja jina iti means wanaweza wakawa washazoea kitu kilichotajwa nataka iwe siri na special”.
MSIKILIZE HAPA

Post a Comment

 
Top