Menu
 Hitmaker wa Lava Lava SHAA amesema wasanii wote hususani wa jinsia ya kike wanapaswa kutafuta menejimenti za uhakika zenye lengo la kumwendeleza msanii aweze kunufaika na kipato cha kazi zake na si kupoteza utu wao kwa kutoa rushwa ya ngono ili kutoka kimuziki.

SHAA ameeleza hayo wakati akipiga stori na kipengele cha Chumba Cha Sindano kupitia kipindi cha Kali za Bomba cha kituo cha redio Bomba FM cha jijini Mbeya  huku akijivunia hatua yake ya mafanikio  ya muziki aliyoyafikia.

    “Mambo mengi ambayo na amini kwa wasanii wengi wa kike ambao hawapo kwenye kampuni  kwa sababu wanajimeneji wenyewe  labda  wanajisimamia wao wenyewe wanakutana  nayo, kama ishu za sijui kutongozwa mara sijui mtu anakuambia hakupi show au wimbo wako hata upiga hadi makubaliano mengine huwa inawakuta . Mimi bahati nzuri sana niko chini ya kampuni na kwa sasa usimamizi wangu ni  Mkubwa na Wanaye ambao ni FELLA na BABU TALE, kwa hiyo nadhani yale majanga niyaite yote (anacheka), sikutani nayo kwa sababu ninayo timu inayojua biashara vilevile ni watoto wa kiume mwisho wa siku hawawezi kuzinguliwa, lakini naamini  kabisa Shaa kama Shaa angekuwa anajisimamia yeye mwenyewe hayo majanga hata mimi yangenikuta sana” alisema SHAA.

   Hata hivyo SHAA hakuishia hapo na kutoa ushauri kwa wasanii wenzake wa Kike kutopoteza utu wao, “Jaribu kutafuta menejimenti, kampuni ambayo kweli ipo pale kwa ajili ya kutengeneza hela na kukuendeleza wewe kama msanii, sio kampuni hizi ambazo ni vivuli kwamba ni Meneja lakini ofisi wapi? Chumbani kwake hapana tafuta kampuni ambayo kweli kampuni ofisi kweli ofisi kwa hiyo ndo ushauri wangu wa bure ambao naona kama kwangu mimi umenifikisha hadi leo hii hapa nilipofika najua kwamba hata msanii mwingine yeyote awe wa kike au wakiume itamfikisha na yeye hukohuko. ”
BOFYA HAPA KUMSIKILIZA.

Post a Comment

 
Top