Menu
 Hitmaker wa Sina Imani SHETTA amesema toka kujiondoa katika Kundi la DAR STAMINA muziki unamlipa kutokana na kipato anachokipata kinakidhi kuendesha na maisha yake na familia kwa ujumla.Akizungumza na Chumba Cha Sindano kupitia kipindi cha Kali za Bomba cha kituo cha redio Bomba FM Mbeya, SHETTA anasemaUkiwa alone unafanya kuwa maisha yako ya kimuziki hela ya muziki unaiona na vitu kama hivyo, kwenye kundi sio kama unaiona lakini inakuja taratibu taratibu sana kwa hiyo mimi kutoka kwenye kundi nikachukua uamuzi sahihi nikaona maisha yanabadilika kwa hiyo ndo faida”.Akizungumzia  sababu iliyomfanya kuandika Track ya Sina Imani aliyomshirikisha Rich Mavoko hapa SHETTA anafunguka “Nilikuwa nimeambiwa naimba sana mapenzi sasa watu walikuwa wanashindwa kuelewa unaweza kumba mapenzi katika kuelimisha na kuburudisha watu wakapata somo na ku-enjoy pia, Nimechokwa wakazungumzia Mdananda, wakazungumzia Nidanganye, Bonge la Bwana. Lakini Sina Imani imekuja ya mapenzi ina ujumbe ndani yake kitofauti kama kucheza kwa sababu ngoma inachezwa Club, inachezwa wapi lakini sometimes ukachill ukisikiliza kwa makini unaelimika kwa hiyo this time nabadilika badilika kwa sababu mimi nimbunifu toka nilipotoka na chochote mimi nachohisi kwa muda huu kinaweza kuwa ni biashara nakikawa kizuri huwa nakifanyaga”.Hapa SHETTA alipoulizwa ana hisi anakitu gani cha utofauti na wasanii wengine “Nikuwa tofauti na watu wanao-rap kwa sababu mimi na Rap lakini na Rap Commercial, kitu ambacho naweza kurap katika beat ya wasanii wanaoimba. Nimefanya nyimbo nyingi kuna nyimbo mpya ya AB SKILLZ, kuna niliyofanya na ALLY KIBA ambapo mimi nime-rap, nina nyimbo na Msanii kutoka Kenya naye beat hizo hizo za kuimbaimba alikuja tu halafu MANECKY akamwambia halo hii beat inatakiwa aimbe SHETTA na vitu kama hivyo kwa hiyo kuna beat hata zikipigwa lazima utasema lazima SHETTA afanye kutokana na ile style ambayo niliiangalia nikaicreate kwa upande wangu na Rap ambapo anaweza kusikiliza mtu yeyote awe mtoto wa kike(msichana) haijamlenga kwamba yaani hii ni wagumu tu Rap yangu mwanaume, mwanamke, mtoto wote wanapenda that’s why inakuwa hivyo.
BOFYA HAPA KUMSIKILIZA

Post a Comment

 
Top