Menu
 


Rapper YOUNG TUSO a.k.a The Ambassador of Temeke Mtoni kwa Aziz Ally ameeleza  kuna tofauti kati ya kuandika na kutunga mashairi ya muziki katika kufikisha ujumbe kwenye jamii, ambapo kuandika huelezea uhalisia wa jambo/tukio na kutunga ni kuzungumzia jambo la kufikirika ambalo halijatokea.Akipiga stori na Kipengele cha Chumba Cha Sindano kupitia kipindi Kali za Bomba cha Kituo cha redio Bomba FM 104.0MHz Mbeya, YOUNG TUSO anasema “Unajua kuna kutunga wimbo na kuandika wimbo kwa tafsiri yangu mimi, kutunga something you create unajua unaweza ukaimage  hivi kwamba lets say kama wimbo wa Mwangwea Rest in peace to him aliimba ile Ghetto langu lakini ukiangalia aliimagination tu  haikuwa ghetto kweli la vile wala halikuwepo ila yeye ali-image unajua  sasa ile naweza kuita alitunga(pale alitunga), Sasa kuandika ni kitu kipo wewe unachofanya unakichukua unakiandika katika mashairi  unaweka pale. Nikizungumzia labda wimbo wangu ule uliofanywa na Mwana FA(Bado niponipo) nilichokifanya unajua Mwana FA was inspired me, Mimi Mwana FA, Proffesa Jay na Fid Q wa mwanza ndio watu ambao waliniinspire sasa nachokifanya ni kwamba sometimes najaribu kupita tu kwenye zile njia zao ambazo wao walizipita kuonyesha kwamba there have done good and na mimi pia nakuwa inspired kufanya kitu kwaajili ya wao”.Akiendelea kutolea mfano ngoma yake ya WAALIMU na hapa YOUNG TUSO anaendelea kutoa ufafanuzi “Kwa hiyo kwanza naweza kusema ni kuandika kwa tafsiri yangu naandika kitu ambacho pengine kipo nakiambia kama WAALIMU, Walimu ni kile kilio kipo kila mtu anajua, unajua always walimu wanalia mishahara mdogo kwa hiyo ule niliandika wimbo sikutunga,kutunga ni kitu  pengine ambacho hakipo unajaribu kuki-image kwa hiyo niliandika. Firstly ni kwamba naandika  nyimbo badala  ya kutunga kwa tafsiri yangu nafikiri nitakuwa nimeeleweka halafu Secondly ni kwamba tofauti ambacho mtu akisikia pengine mtu asikie mara moja lakini ikipita wiki mbili baadae ukaja mtu kama Chris Bee ukamwambia kwamba Eee! Bwana kuna mtu fulani alitoa wimbo siku fulani unajua wewe unakumbuka nilipata kuusikia siku fulani ukakumbuka aaah bwana nimepata  kuusikia siku moja huwezi kuamini kuna watu nakutana nao wananiambia mbona mimi niliwahi kuusikia wimbo wako siku moja tu lakini inapita miezi mitatu wanakuambia ndio nakumbuka nilishawahi kuusikia  sasa ukifanya wimbo ambao hauko tofauti watu wanaweza kuusikia na wala wasikumbuke kama walishawahi kuusikia kwa hiyo ni kujaribu kutafuta kitu cha tofauti hivi na kukileta katika jamii”.
 MSIKILIZE HAPA ZAIDI.Hata hivyo YOUNG TUSO anatarajia kuachia ngoma mpya inaitwa Tunadisturb The Peace By Young Tuso Feat. Ney Wa Mitego! ngoma inatoka studio ya Uprize Muzic chini ya mtayarishaji Dupy Lilay James!.

Post a Comment

 
Top