Menu
 

Na, Mwandishi wetu.
Waziri wa Afya na Utawi wa Jamii Dokta Hussen Mwinyi amezindua kitabu za horodha ya dawa muhimu pamoja na matibabu yake huku akiwataka  Madaktari na Wafamasia kuhakikisha wanatoa dawa sahihi kwa wagonjwa ambazo zipo ndani ya muda na sio zile ambazo muda wake umekwisha.


Agizo hilo limetolewa na waziri huyo wakati akizindua kitabu hicho jijini Dar es Salaam.


Dokta Mwinyi amesema kuwa unapotumia dawa zaidi ya unapotakiwa inaweza kupelekea usugu wa vimelea ambapo jambo ambalo ni tatizo kubwa ndani ya jamii. 
 

Pia amesema kuna haja sasa ya kila daktari na wafamasia kutoka mikoa yote nchini kuhakikisha wanafuata taratibu, kanuni na sheria zilizopo ili waweze kutekeleza wajibu wao vizuri kwa kutoa tiba ya dawa sahihi zinazotakiwa kwa mgonjwa na sio kumrundikia dawa mgonjwa ambazo aendani na ugonjwa anaoumwa.


Aidha amewata watoa dawa katika mahospitali na maduka ya dawa za bianadamu kufuata muongozi muhimu wa kitabu kilichotolewa kinachoonyesha  matumizi ya dawa sahihi zinazotakiwa kutolewa kwa wagonjwa wanaosumbuliwa na maradhi mbalimbali ya kiafya.


Amesema madhumuni makubwa ya kuwa na horodha ya dawa muhimu ni kuelekeza watoaji wa dawa kujua wajibu wao wa kutumia dawa maalumu ambazo zipo ndani ya horodha hizo na si vinginevyo.


Katika uzinduzi huo umehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa serikali, madaktari wadau kutoka sekta ya Afya pamoja na wadau kutoka mashirika yasiyo ya kiserikali nchini.

Post a Comment

 
Top