Menu
 


Mwenyekiti wa klabu ya Simba Ismail Aden Rage amewashukuru wanachama pamoja na mashabiki wa klabu hiyo kufuatia ushindi wa mabao matatu kwa moja walioupata mwishoni mwa juma lililopita dhidi ya mahasimu wao Dar es salaam Young Africans katika uwanja wa taifa jijini Dar es salaam.

Ismail Aden Rage amesema siri kubwa ya mafanikio ya ushindi huo ana hakika imetokana na mshikamano ulioopo ndani ya klabu ya Simba licha ya mgogoro unaendelea kuzizima kufuatia baadhi ya wanachama kumtaka atangaze kujiuzuulu.

Hata hivyo Ismail Aden Rage akarejesha salamu kwa viongozi wa klabu ya Dar es salaam Young Africans kufutia pongezi za ushindi walizozitoa kwa Simba ambapo amesema suala la kikosi chao kucheza soka safi ni kawaida endapo hakutokua na tatizo la kuhujumiana.

Wakati huo huo raisi wa TFF Jamal Malinzi amesema suala la mgogoro unaendelea ndani ya klabu ya Simba linaendelea kufanyiwa kazi baada ya mwenyekiti Ismail Aden Rage kuomba maamuzi yaliyochukuliwa na kamati ya utendaji ya kutaka kuitishwa kwa mkutano wa wanachama ndani ya siku 14 ambazo tayari zimeshakwisha.

Post a Comment

 
Top