Menu
 


Katibu mkuu wa shirikisho la soka nchini TFF Celestine Mwesigwa amesema hafikirii kulipiza kisasi kwa viongozi wa klabu bingwa Tanzania bara Dar es salaam Young Africans kufutia sakata la kufuta kazi mwezi Oktoba mwaka 2012.

Mwesigwa ambae alitambulishwa kwa waandishi wa habari siku mbili zilizopiuta amesema atahakikisha anafanya kazi ya ukatibu wa TFF kwa kufuata uweledi na si kuanza kufikiria ni nani alimfanyia mabaya siku za nyuma.

Amesema TFF ni taasisi ya soka inayoshughulika na mchezo huo nchi nzima na si klabu ya Dar es salaam Young Africans pekee.


Kwa upande wa raisi wa TFF Jamal Emil Malinzi nae amelizungumzia sakata hilo kwa kina kwa kusema mpaka wamefikia hatua ya kumpa ajira Celestine Mwesigwa kuwa katibu mkuu wamefuatilia kwa kina nini kilichotokea ndani ya klabu ya Dar es salaam Young Africans na wamejiridhishwa na kile walichokiona.


Post a Comment

 
Top