Menu
 


Hitmaker wa Roho Yangu RICH MAVOKO ameeleza kuwa yeyeni Msanii pekee kuleta Rate Camera nchini Tanzania licha ya kumgharimu pesa nyingi lakini hakujali kwa sababu anataka kupata video yenye ubora wa kimatifa na ametoa kwa Wasanii wanao-hit  kuwatumia Madirector wa video wazawa ili kuwatangaza.Nimemchukua Director mtanzania ndiye atakaye direct video , lakini watu watakao shoot video ni wale Waganda na Wakenya, halafu kwa mara ya kwanza Msanii wa Bongo Fleva anayeleta  Rate Camera  kwa Tanzania ni mimi hapakuileta imenigharimu lakini  kwa sababu nilikuwa nataka picha yenye quality. Soon video itatoka nataka nilichokiimba kili-relate na video ndio maana inakuwa inanipa wakati mgumu  sitaki  nionekane nilichokiimba kiwe kime–oversize video.” RICH MAVOKO alikiambia kipengele cha Chumba Cha Sindano cha Kipindi cha Kali za Bomba cha redio Bomba FM Mbeya.Na vipi kuhusu gharama  halisi video ya Roho Yangu hadi kukamilika?, RICH MAVOKO anafunguka zaidi, “Itagharimu hela nyingi kama milioni 10 na kitu mpaka sasa hivi  kwa hiyo bado hatujamaliza baadhi ya shot za mwisho mwisho baada ya hapo nitapata bajeti nzima, kuna watu inabidi tuwachukue, magari tuyachukue na kuna baadhi ya location bado hatujaenda kuchukua”.Kwa hatua nyingine RICH MAVOKO ametoa wito kwa watanzania wote kujivunia uzalendo ili kufikia soko la ushindani la kimataifa “Kiukweli hii ni kwa watanzania wote wanatakiwa wajivunie nchi, nimejaribu kufanya production ya audio ni Mtanzania, Director wa video wa Tanzania ambaye alikuwa tayari kufanya hiki kitu ndio maana mimi nimeamua kumchukua Director mtanzania ili kufanya video yangu hawa watatoka lini kama tusiposapotiana. Wenzetu Wanigeria wanafanya hivyo wanachukua Ma-director wa Kinageria sio kwamba wanashindwa kuwalipa Madirector wa Kimataifa kama Carlyon Taylor lakini wanafanya wao kama wanigeria ili kutangaza taifa lao”.
 BOFYA HAPA KUMSIKILIZA ZAIDI.. 

Post a Comment

 
Top