Menu
 


Kundi la WA2KU2 lenye masikani yake Jijini Tanga, linaloundwa na JOHN WALKER na RAS LION lipo mbioni kuachia vipindi vya Comedy katika vituo vya Televisheni nchini baada ya kuwa kimya kwa muda mrefu nah ii ni kutokana na mashabiki wao kuwataka wafanye Comedy.

Crew Member wa Wa2ku2 hilo JOHN WALKER amefunguka na taarifa hiyo rasmi kupitia Kipengele cha Chumba Cha Sindano kupitia kipindi cha Kali za Bomba cha kituo cha redio Bomba FM 104.0MHz Mbeya.

“Tulikuwa kimya kwa muda mrefu kwa sababu tulikuwa kwa sababu kuna mambo mengine tulikuwa tunafanya, sasa hivi tumeingia kwenye Comedy pia, kwa hiyo tulikuwa Arusha tumeweka kambi kwa sababu ya kurekodi vipindi vyetu vya komedi muda wote huo. Kwa hiyo tumesharekodi vipindi vingi  na sasa tupo kwenye hatua za mwisho ambazo kuna baadhi ya TV tumepeleka DEMO zetu tupo kwenye maongezi ya mwisho kwa hiyo watu wanaweza kuziona kwenye TV” alisema JOHN WALKER.

Kwa hatua nyingine JOHN WALKER ameelezea juu ya uamuzi wa kufanya Comedy na nini kilicho wasukuma kufanya hivyo “Kilichotufanya tufanye Comedy ni maoni ya watu unajua ukifuatilia nyimbo zetu nyingi zinakuwa na ujumbe na vichekesho ndani yake, Watu wakasema mnaweza kufanya hata Comedy  kwa hiyo unafanya na upande wa pili kuingiza kipato pia”.

Hata hivyo JOHN WALKER ameelezea ujio wa ngoma yao mpya ya Mkora iliyopikwa katika studio la Grandmaster na siri ya kundi lao kudumu “Kundi letu lipo vilevile halijawahi kuvunjika toka tuungane miaka kumi iliyopita ndio maana tunaendelea kutoa ngoma kwa pamoja, ni kundi pekee lilodumu kwa muda mrefu mimi(JOHN WALKER) na RAS LION tumekuwa kama ndugu, ndugu wanaweza kugombana lakini undugu hauwezi kufa siri kubwa kuwa muwazi na mkweli”
BOFYA HAPA KUMSIKILIZA ZAIDI.

Post a Comment

 
Top