Menu
 Wauza mitumba wa Ilala Ashanti United wamethibitisha taarifa za kukamilisha mpango wa kumpa ajira King Abdallah Kibaden Mputa ambae tayari ameshaachana na klabu ya Simba.

Afisa habari wa klabu ya Ashanti Utd Rajab Marijan amesema watakua na Kibaden kama mkuu wa benchi la ufundi hadi mwishoni mwa msimu huu huku wakiamini uwezo wa kocha huyo utakisaidia kikosi chao kufikia melngo ya kufanya vyema katika duru la pili la ligi kuu ya soka Tanzania bara.


Katika hatua nyingine Rajab Marijan amesema wamefurahishwa na kitendo cha kizalendo ambacho kimeonyeshwa na kocha Hassan banyai ambae amekua mstari wa mbele kumpigia upatu King Abdallah kibaden ili aweze kupewa kibarua huko Ilala.


Hata hivyo dalili za kibaden kujiunga na Ashanti utd zilianza kuonekana tangu alipokiri kupokea barua ya kusitishiwa mkataba wake na klabu ya Simba.

Post a Comment

 
Top