Menu
 Hitmaker wa Haina Ngwasu STEREO atafunga mwaka 2013 kwa kufanya mambo makubwa mawili, ikiwa ni pamoja na kuachia ngoma mpya aliyoifanya kwa miondoko tofauti na Hiphop kwa madai ya kuendana na soko la ushindani kwa na anatarajia kushoot video ya ngoma ya Haina Ngwasu.

STEREO amepiga Stori na kipengele cha Chumba Cha Sindano kupitia kipindi cha Kali za Bomba cha kituo cha redio Bomba FM kilichopo jijini Mbeya.

 "Tahere 18 mwezi huu wa 12 tunatarajia ku-shoot video yangu ya Haina Ngwasu  tuta-shoot na jamaa mmoja anaitwa Meck, kampuni yake inaitwa Ngome Video, ni kampuni nzuri haijafanya video nyingi sana lakini ina video kali na Mwezi wa 12 kabla haujaisha kabisa STEREO atakuja na OMMY DIMPOZ sio kwa miondoka ya HipHop, tunahama kidogokidogo(kwa msisitizo) sio sana tunajaribu kuona na soko jingine pia linasmaje" Alisema STEREO.

Hata hivyo alipoulizwa Video hiyo ya Haina Ngwasu itagharimu kiasi gani cha pesa hadi kukamilia? STEREO hapa anafafanua, "Kulingana na Script ilivyokaa sasa kuna vitu vingine bado, kuna Logistics tunafanya ili kuweza kupatikana na gharama halisi ya shughuli nzima kwa hiyo nafikiri ikishaisha ndio nitakuwa katika position na kusema video imenigharimu kiasi gani". 
BOFYA HAPA KUMSIKILIZA ZAIDI. 

Post a Comment

 
Top