Menu
 


Rapper Mike Mwakatundu a.k.a MIKE TEE ameweka wazi kuwa atakuwa akimtumia msanii mwenzake wa Hiphop Bongo STEREO kama mtunzi wa mashairi ya nyimbo zake na kuwatosa wasanii wakongwe ambao walikuwa wakimuandikia huku akitarajia kutoa nyimbo mpya kila mwisho wa mwezi baada ya kujiajiri.

MIKE TEE amepiga stori na kipengele cha Chumba Cha Sindano kupitia kipindi cha Kali za Bomba cha redio Bomba FM Mbeya kuwa amesoma alama za nyakati na kwamba muziki wa sasa unahitaji mabadiliko makubwa.

 "Sasa hivi na change kitu kikubwa nimejaribu kubadilisha writers wa muziki wangu, kwa sababu mara ya kwanza nilikuwa namtumia ADILI, nimemtumia MWANA FA, nimemtumia FID Q kwa sasa hivi nimetumia hawa vijana tusema wapya sasa hivi namtumia sana STEREO. Kwa hiyo nadhani hata ukiangalia atyle ya muziki wa kwangu huu wimbo niliofanya na JUMA NATURE nimefanya tofauti kwa hiyo sitaki watu wa-creme alikuwa hivi na hivi, kweli nilisema sintobadilika lakini nawaambia sijabadilika nimekua" alifunguka MIKE TEE.

Hata hivyo MIKE TEE ameelezea sababu za kuamua kumtumia STEREO katika uandishi wa mashairi na asiwatumie wasanii wengine "Unajua wale wanafanya muziki tofauti na mimi, nimekucha kumchukua STEREO kwa sababu anafanya HIPHOPna mimi nafanya Hiphop, yaani ni mtu ambaye nimemchukua ambaye kitu cha kwanza ukimuuliza STEREO ni Fan wangu wa siku nyingi kabla hajaanza music alikuwa anasikiliza sana nyimbo zangu kwa hiyo naangalia kwanza nani yupo karibu na mimi nani anaweza kukifanya kitu ambacho mimi nakihitaji".

BOFYA HAPA KUMSIKILIZA ZAIDI.

Post a Comment

 
Top