Menu
 Hitmaker wa Sitaki Kuumizwa SAJNA amesema kuwa muziki sio kuimba tu ila ni kutengeneza nyimbo ambazo zitakuwa zinadumu kwa kipindi kirefu kuanzia miezi sita na zaidi, kutokana na ujumbe mzito wa mashairi tnaotoa mafunzo ndani ya jamii na sio wenye kusababisha mmomonyoko wa maadili.

SAJNA akipiga Srori na Chumba Cha Sindano kupitia Kipindi cha Kali za Bomba cha redio Bomba FM Mbeya, amesema familia yake na Bosi wake hulazimika kuingilia kati na kumtaka kufanya muziki ambao utamfanya mdau wa muziki kuwa na shauku ya kusikiliza mara kwa mara ujumbe unaopatikana katika nyimbo zake.

 “Hata mama yangu alishaniambia, dada yangu, kaka yangu umeona nyimbo za zamani za akina Mubaraka Mwishehe na mwengineo sio kwamba wamekufa ndio zinafanya vizuri hapana hata leo akisikiliza mtu fulani anapata ujumbe kutokana na kutengeneza wimbo wenye uhalisia, huwa wananikumbusha kuwa unaiona Iveta yako ulivyoitengeneza ina uhai, Sitaki kuumizwa, Mganga ni wimbo ambao kila mtu akiusikiliza lazima imkumbushe kitu fulani” alisema SAJNA.

Kwa upande mwingine SAJNA ameeleza sababu za ukimya wake na kuwatoa hofu mashabiki wake kuwa wakae mkao wa kula kwani yupo jijini Dar es salaa, kwa ajili ya kutengeneza project moja kwa mshikaji wangu JAMES na nyingine kwa Man Water,“Kuna kipindi nilikuwa School, mshoni wa mwezi huu wategemee kitu kizuri kuna kipindi nasikia Bosi wangu anakuwa na majukumu ya kazi lakini navuta subira mpaka amalize majukumu lakini bado msaada wa TETEMESHA upo palepale. Najitahidi kutengeneza wimbo ambao utanifanya kila mtu akisikiliza ajue kuna SAJNA sio anasikiliza anaweka anainuka unaona(kwa msisitizo) anatakiwa anasikiliza na anapata ujumbe anakuwa anasema SAJNA amefanya kitu kizuri cha kugusa jamii”.
BOFYA HAPA KUMSIKILIZA ZAIDI..

Post a Comment

 
Top