Menu
 


Kufuatia kuandamwa na Magazeti pendwa Rais wa Masharobaro na Hitmaker wa Bashasha Raheem Ramadhani a.k.a BOB JUNIOR amesema kuwa licha ya kuandikwa vibaya kwa kile alichokidai kuwa ni udhalilishaji dhidi yake, amekuwa akienda kushitaki kwenye vyombo vya dola lakini hasikilizwi.

 Akipiga Stori na kipengele cha Chumba Cha Sindano kupitia kipindi cha Kali za Bomba hapa Bomba FM Mbeya, BOB JUNIOR amesema kutokana na kutosikilizwa amekuwa akikosa njia mbadala yakupata haki yake.

"Hata ukitaka kuweza kushitaki hausikilizwi yaani hata haieleweki haileweki yaani wee acha tu(kwa msisitizo), mengi siku zote magazeti yamekuwa yananiandika tu hovyo... hovyo... hovyo... hata sijui wanajiandikia tu. Wewe angalia hata magazeti ya Kiu utaona, magazeti ya wiki iliyopita wamenichoresha mimi siku zote".

Kwa upande mwingine BOB JUNIOR alipouliza anahisi ni kwanini amekuwa akiandamwa yeye tu na wasiandame wasanii wengine alitoa utetezi huu akihusisha na biashara, "Aaaah bwana wee unajua mtu ukishakuwa juu umenielewa bwana wewe angalia mtu yeyote yaani akishakuwa juu tu yaani ndio inavyokuwa wenyewe ndio wanaona sijui ni biashara kwao, wanaweza kutafuta vistori vingine vinahusiana na ukweli vingine vya uongo basi hizo za uongo wataziandia sana wataziforce ziwe za ukweli".

BOFYA HAPA KUMSIKILIZA ZAIDI.

Post a Comment

 
Top