Menu
 

Bwana harusi akiwa na mpambe wake kanisani wakimsubiri bibi Harusi
Jamaa wameshika vichwa hali haieleweki


Bi Harusi Naomi Ngoje akiwa amejilalia chumbani akiwa anahuzunika na kushangaa wazazi wake kurudisha mahali ya mchumba wakeHABARI zilizotufikia hivi punde kutoka nyumbani kwa familia ya Bi harusi ambayo ilikuwa ikipinga ndoa isifungwe kutokana na Bwana harusi kushindwa kumalizia sehemu ya Mahari zinadai kuwa ndoa imevunjwa rasmi na kilichobaki ni mzozo wa kurudishiana fedha.

Pande hizo mbili ya Kiume na Kike zimengia kwenye Mzozo na kuvutana kuhusu fedha baada ya Wazazi wa Mwanamke kukubali kurudisha fedha hizo pamoja na vitu walivyopokea huku kikubwa kikiwa ni upande wa Mwanaume kudai wapewe papo hapo.

Vitu vinavyodaiwa ni Fedha taslimu takribani Shilingi 310,000/= ambazo zilitolewa kwa ajili ya Mkaja pamoja na kiingilio, Blanketi na Mashuka.

Kwa habari zaidi endelea kufuatilia mtandao wako huu ambapo mpaka sasa zaidi ya shilingi 50,ooo zimechangwa na ndugu wa Mume na kujaribu kuziwasilisha kwa ndugu wa Bibi harusi hata hivyo ndugu hao wamekataa kuzipokea.

Kwa habari zaidi Jumatatu endelea kufuatlia.


Na Ezekiel Kamanga, Mbeya

ENDELEA KU - LIKE PAGE YETU YA MWANDISHI WA BLOGU HII.

Post a Comment

 
Top