Menu
 


Mwenyekiti wa klabu ya Simba Ismail Aden Rage amewataka wanachama pamoja na mashabiki wa klabu hiyo kujifunza kusamehe kama yeye alivyokubali kuwasamehe wajumbe wa kamati ya utendaji kwa namna ya walivyomfanyia.

Ismail Aden Rage ambae anashurutishwa kutangaza kujiuzulu nafasi yake klabuni hapo amesema kuna haja sasa kwa wartu wa Simba kubadilika na kutazama namna ya kuisaidia klabu yao ili isonge mbele na kufikiria kulipiziana visasi halia mbayo haijengi.

Katika hatua nyingine Ismail Aden Rage ameonyesha kutofurahishwa na utaratibu uliotumika wa kumuondoa aliekua kocha wa kikosi cha Simba King Abdallah Kibaden kwa kusema haikutumika busara njema kwa kocha huyo kuondoka klabuni hapo.

Rage amesema King Abdallah Kibaden hakustahili kuondolewa kama mtu ambae hajulikanda ndani ya klabu ya Simba na badala yake ungetumika utaratibu mwingine wa kibusara wa kumuondoa.


Hata hivyo tayari King Abdallah Kibaden alimuomba mwenyekiti wa klabu ay Simba Ismail Aden Rage kuacha msimamo wa kung’ang’ania baada ya viongozi wenzake kukubaliana kumuondoka kwenye benchi la ufundi la wekundu wa Msimbazi Simba.

Post a Comment

 
Top