Menu
 


Hatimae shirikisho la soka nchini TFF limethibitisha taarifa za kumuajiri Celestine Mwesigwa kuwa katibu mkuu wa shirikisho hilo baada ya kamati ya utendaji kukutana mwishoni mwa juma lililopita na kupitia maombi ya wadau mbali mbali waliokua wamewasilisha maombi ya kuwaiwania nafasi hiyo.

Raisi wa TFF Jamal Malinzi amesema kuajiriwa kwa Celestine Mwesigwa kumezingatia vigezo na taratibu walizokua wameziainisha kwenye tangazo la ajira hivyo ataanza kazi zake mwanzoni mwa mwaka 2014.

Jamali Malinzi pia amethibitisha ajira ya mkurugenzi wa vyama wanachama na masuala ya kisheria wa TFF ambayo imekwenda kwa aliekua katibu mkuu wa klabu ya Evodius Mtawala .

Pamoja na kuthibitisha taarifa za nafasi hizo mbili za ajira raisi wa TFF akatangaza maamuzi ya kamati ya utendaji ambayo yamechukuliwa katika nafasi nyingine za ajira ambazo zilitangazwa mwezi uliopita.
   
Baada ya thibitisho huo katibu mkuu wa TFF Celestine Mwesigwa akazungumza na waandishi wa habari ambapo amesema anatambua majukumu aliyonayo kwa sasa ni makubwa hivyo hana budi kuutumikia mpira wa Tanzania kikamilifu kwa ajili ya kutimiza malengo yanayokusudiwa na uongozi mpya wa shirikisho hilo.
   
Nae mkurugenzi wa vyama wanachama na masuala ya kisheria wa TFF Evodius Mtawala amesema atafanya kazi kwa uadilifi mkubwa kufitia kanuni na taratibu zilizowekwa hivyo ana hakika kila jambo litakwenda sawia.
   

Wakati huo huo raisi wa TFF Jamali malinzi ametangaza kamati ya uchaguzi pamoja na kamati ya rufaa ya uchaguzi huku akiahidi kutangaza kamati nyingine za kisheria siku chache zijazo.

Post a Comment

 
Top