Menu
 


JAMII ya watoto yatima imeshauriwa kutokatishwa tamaa na maisha magumu yanayoikabili badala yake iendelee kushirikiana na wadau wanaoijali katika kutafuta ufumbuzi wa changamoto zinazoikabili.

 Kauli hiyo imetolewa na mkuu wa Dawati la Ukatili na Unyanyasaji wa kijinsia la polisi mkoa wa Mbeya SAMORA SARANGA wakati akizungumza na watoto yatima wanaolelewa katika kituo cha Malezi na Matunzo ya watoto Yatima cha Msamaria Mwema kilichopo Songwe wilayani Mbeya.

 Aidha ameitaka jamii inayowazunguka yatima kutimiza wajibu wake kwa kuwajali watoto hao na kuwasaidia kufikia malengo yao.

 Naye mmoja wajumbe wa dawati hilo MARY GUMBO amesema dawati limebaini uwepo wa watoto wengi waliopo kwenye mazingira magumu licha ya uwepo wa wazazi wa karibu walio na uwezo wa kuwalea.

Post a Comment

 
Top