Menu
 

Hitmaker wa Bomoa Bomoa BABY J ametoa wito kwa vioo vya jamii hasa wasanii wa kike waliopo katika tasnia ya muziki na filamu kutojihusisha na biashara haramu ya madawa ya kulevya kwani wanaidhalilisha nchi yetu.

 

 “Well kusema ukweli siwezi kuingilia sana kwa hilo kwa sababu kila mtu anafanya kitu kupitia yeye mwenyewe na plan zake za maisha yake, lakini kiukweli kama mwanamke au kama kioo cha jamii sio kitu vizuri kwa sababu tunachafua majina yetu na pia tunaipeleka vibaya tasnia zetu hata hivyo tunakandamiza taifa letu la baadae(vijana)” alisema BABY J kupitia Kipengele cha Chumba Cha Sindano cha Bomba Base Show kipindi kinachoruka hewani Bomba Fm Radio.

 

Aidha BABY J amesema jamii inapaswa kuwa makini na maisha ya sasa kutokana na dunia kubadilika “Kusema kweli kitu kikubwa nachoweza kukiongea najua watasikiliza Wazee, vijana na watoto nafikiri kitu kikubwa nachokizungumza ni kwamba binadamu wenzangu wote tuwemakini kwa sababu sasa hivi dunia kidogo ime-change kuna magonjwa/maradhi hatari hii na maanisha kwa walio izidi au niliowazidi mimi au tulio kwenye same age tuwe makini na hii hali”.

 

Kwa hatua nyingine BABY J amezungumzia ujio wake “Kitu kingine napenda kuwaambia mashabiki wangu wakae tayari kwa sababu sasa hivi ni mwaka 2014 kuna vitu vingi vinakuja na watavifurahia kwa hiyo wavipokee, kuna wimbo natarajia kuuachia japo ni mapema sana kuuongelea, well studio ambako nitarekodia ni Akhenato chini ya producer Lil Gheto nafikiri anafahamika”.

Post a Comment

 
Top