Menu
 

Bob Junior katika pozi. 

Hitmaker wa Bashasha  RAHEEM RAMADHAN a.k.a BOB JUNIOR, anatarajia kuusema ukweli wake wote uliozunguka maisha yake ya ndoa iliyovunjika katika wimbo wake mpya alioupa jina la Ukweli Wangu.

Akiongea na Kipengele cha Chumba Cha Sindano kupitia Kipindi cha Bomba Base Show cha redio Bomba FM Mbeya Bob Junior alifunguka hivi “Kuna wimbo unaitwa UKWELI WANGU mwezi wa pili au mwezi wa tatu nitauachia lakini umeshaisha  upo Mastered na kila kitu ni wimbo mmoja mkali sana unahusu ukweli wa maisha yangu juu ya mami na mapenzi yangu yote ni mambo mengi nimeongelea na wimbo wa feeling sana”

VIPI KUHUSU VIDEO YA BASHASHA?
Hata hivyo amesema kuwa booked na u-busy wa majukumu  kwa Ma-Director(waongozaji) wa Video kupitia kampuni ya Ogopa Videoz ya nchini Kenya ni sababu kuu iliyochangia video ya BASHASHA kuchelewa kutoka mpaka sasa.

“Video nimepewa nusu demo mpaka sasa hivi, jamaa wamesafiri wapo Marekani kuna project wanaifanya na Wakenya Fulani, wakirudi nadhani deadline next week wamesema watanipa full video, wamenifanya ni delay sana sasa sijui kwamba project yangu watakuwa wameimaliza na kunipa” alisema Bob Junior.


Post a Comment

 
Top