Menu
 

Mkali wa miondoko ya Reggae na Dancehall kutoka Bongo DEDDY ameelezea imani yake kuwa aina hiyo ya muziki utamfikisha katika nyanja za kimataifa kutokana na kuchanganya fleva za kikwetu na za wasanii wa kimataifa kama SEAN PAUL, BEEN MAN na wengineo.

 

Akifunguka kupitia Kipengele cha Chumba Cha Sindano cha Bomba Base Show kipindi kinachoruka hewani Bomba Fm Radio, DEDDY alisikika kwa kauli hii “Vitu tofauti mashabiki watarajie kutoka kwangu kwa sababu ya mimi kuimba katika aina tofauti ya muziki wa Reggae na Dancehall, track ambazo zitakuja zitakuwa na different kind of fleva”

 

“Kwa sababu ni kitu tu ambacho hatujakizoea huku tumezoea kusikiliza muziki tu wa aina fulani, kama sisi tumeweza kuwasikiliza akina SEAN PAUL, BEEN MAN kitambo hicho na tukacheza vizuri miziki yao mimi nikaendeleza aina yangu ya muziki wenye fleva kama ile kikwetu zaidi inaweza kunifikisha mbali zaidi kimataifa” Aliongeza DEDDY kwa msisitizo.

 

Hata hivyo DEDDY ameelezea nini kilichomsukuma kufanya aina hiyo ya muziki licha ya wasanii wengi Nchini kujikita katika Hiphop, Zouk, Rnb na Afro Pop? “Katika kuwa na upendo wa kusikiliza aina tofauti ya miziki Reggae ilikuwa ni moja ya muziki ulionikaa sana kichwani kwa sababu back n days nilikuwa naweza ku-perform hizo nyimbo kwa hiyo nilikuwa najifunza kufanya aina nyingine za muziki still bado Reggae ilikuwa imenikaa sana nikaona si mbaya zaidi ni kitu cha utofauti naweza kukifanya na kwetu kikawa na mwamko fulani lets me do it”.

Post a Comment

 
Top