Menu
 

Crew members wa Wakacha Warriors Flo(kushoto), Cyril a.k.a Kamikaze(katikati) na Jux(Kulia)


Crew Member wa Wakacha Warriors Cyril Fransisco a.k.a Kamikaze amedai baada ya ukimya wa muda mrefu mwaka huu 2014 wanavunja ukimya na kuwa jirani na mashabiki wao kwa kutoa ngoma mpya na video watakayoanza kushoot wiki ijayo.

Akielezea sababu za kuwa kimya  kupitia kipengele cha Chumba Cha Sindano kipindi cha Bomba Base Show cha redio Bomba FM Mbeya Cyril a.k.a Kamikaze alikuwa na haya ya kusema “Ni kwamba mwenzetu Jux alikuwa yupo China akisoma unajua anakwenda na kurudi kwa hiyo timing yetu ilikuwa mbovu kuna mwaka 2011/12 mwanzoni tuliacha ku-introduce Wakacha tu kwa hiyo hatukutoa nyimbo zetu kama solo artist”. 

Akizungumzia mchakato wa kuanza kushoot video yao mpya Kamikaze/Cyril amesema kwa sasa wapo katika mazungumzo na Director Nick Dizzo wa E Media ili a-shoot video hiyo ya wimbo wao uliotengenezwa na Producer Manecky wa AM Records.

“Kama kundi tunafanya video muda si mrefu tuseme kuanzia wiki ijayo, ngoma yetu moja hivi ambayo haijawahi kutoka ni mpya, sasa hivi tunamaongezi na Nick Dizzo nadhani mazungumzo yakikamilika kuanzia wiki ijayo hiyo tutakuwa tunafanya kitu. Nadhani katika Ma-director wa kitanzania ambao ukitaja moja, mbili, tatu na yeye yupo nadhani video zake bora zimeshaonekana nyingi” alisema Cyril.

Kwa hatua nyingine ameongeza kuwa “Nadhani kila ujio wetu mpya kwa mwaka huu 2014 utakuwa wakitofauti kuliko kazi zote tulizowahi kuzifanya na kuziachia kwa sababu najua siku zote muziki ni biashara na kusoma alama za nyakati najua mashabiki wetu wanataka nini na kwa wakati gani”.


Kundi la Wakacha linaundwa na wasanii watatu ambao ni Cyril a.k.a Kamikaze, Jux pamoja na Flo na sokoni wameingiza biashara ya T-shirt na top zenye logo ya jina la kundi lao.

Post a Comment

 
Top