Menu
 


Hitmaker wa Tema Mate tuwachape MADEE ambaye pia ni crew member wa Tiptop Connection ameeleza kuwa baada ya wiki moja track ya Pombe yangu remix itakuwa hewani akiwashirikisha kundi la Pro habo Unit maarufu kwa jina la P Unit kutoka nchini Kenya.

Akifunguka kupitia kupitia kipengele cha Chumba Cha Sindano kipindi cha Bomba Base Show cha redio Bomba FM Mbeya MADEE amesema “Ile ngoma ilitembea vizuri kule Kenya yaani Nairobi imefanya vizuri jamaa wameisikia wakamtafuta AY naye akawadirect kwangu tukaongea kwamba wanataka kufanya collabo na mimi kwa sababu ya remix ya huu wimbo kwa sababu wao pia walikuwa na mashairi kwa hiyo mimi nilichokifanya nikaongea na Marco Chali akakubali akampa beat AY  jamaa wakafanya ikarudishwa huku Dar es salaam tena mimi nimemaliza kuingiza sauti juzi usiku”

Unaimani kuwa jamaa P Unit wanaweza kuitendea haki  na kwenda sambamba na style yako? “Ile pombe yangu ni mtindo wa rap ni mtindo ambao hata P Unit wanafanya ni beat Fulani za kapuka hiyo sio hiphop ni rap ambayo mtu yeyote yule anayerap vizuri anaweza kurap kwenye mdundo kama ule itanifikisha kule ambako napataka siku zote mimi malengo yangu ni kutaka kutanua aina ya muziki wangu kufika ambako watu wengine wamefika”


Je anaizungumziaje P Unit katika Collabo hiyo? “Ukifanya wimbo na watu kama P Unit  ambapo tayari wao wameshatanua muziki wao East Afrika kila mtu atataka kusikiliza huyo wimbo, kila mtu mtu atataka kuangali huyu Madee na P Unit wamefanya nini unajua mimi nimeshika sana Tanzania, Kenya bado sio vizuri sana lakini kwa kufanya nyimbo na wale jamaa basi kila Mkenya atataka kusikiliza nimefanya nini na kunisikiliza na atataka kujua Madee anafanya nini”. 

Post a Comment

 
Top