Menu
 

Mkali wa ngoma ya Mapito MWASITI amesema mkakati mkubwa wa mafanikio  na kudumu katika music industry ni msanii kuchagua aina moja ya muziki ambao unaweza kuufanya na kujifunza zaidi.

 

Akipiga stori kupitia Kipengele cha Chumba Cha Sindano cha Bomba Base Show kipindi kinachoruka hewani Bomba Fm Radio, Mwasiti amesema “Kiukweli mimi huwa siami katika muziki wangu, huo ni mkakati wangu mkubwa sana kwa hiyo mara nyingi mimi simu mtu wa ku-trick sana yaani utanisikia katika staili tatu za miziki mara nyingi huwa naheshimu sana maamuzi yangu ya kikazi na muziki ninao ufanya ni ngumu sana kusema mtu atanishindanisha mimi na msanii mwingine kama mtu akimsikia Mwasiti anamuona mtu mwingine kabisa”.

 
Je, anazungumziaje siri kubwa ya mashabiki juu ya kusapoti muziki? "Ni vizuri kabisa ukajua hii ni biashara watanzania wameshajua kuwa muziki ni biashara, biashara lazima product zikawa zinafanana kwa uso lakini zikawa na ladha tofauti umenielewa lakini mtu anaweza akawa anauza mifuko lakini ukawa unaitwa mfuko wa Rambo, huu wa nini lakini yote tunawekea bidhaa tukinunua dukani kwa hiyo as long as unafanya kazi lakini unajua unataka nini ni ngumu sana hata competition itakuwa inakupa challenge sio kwamba inakutisha nop inakuwa inakupa tu challenge ya kuwa unafikiria unataka nini zaidi katika muziki wako watu waendelee kukusikiliza”

Post a Comment

 
Top