Menu
 


Msanii Tunda Man katika pozi.

Hitmaker wa Msambinungwa  TUNDA MAN amedai kuwa anatarajia kumshirikisha nyota wa miondoko ya Dance kutoka Congo - Kinshasa FALLY IPUPA katika ngoma yake mpya ya Hasara Roho.

“Kuna ngoma inaitwa Hasara Roho nataka kumshirikisha Fally Ipupa, kwa hiyo nasikilizia mpango huo nimeshamtumia Beat na Vocala kwa hiyo nasubiri na yeye anitumia” Alifunguka TUNDA MAN kupitia Kipengele cha Chumba Cha Sindano kupitia kipindi cha Bomba Base Show ya Bomba Fm Radio.

Aidha ameelezea harakati za kukamilisha Video ya Msambinungwa, ambapo audio amemshirikisha ALLY KIBA na hapa anaelezea nini kinachoendelea “AGNES MASONGANGE ndio model wa Msambinungwa kwa hiyo atashoot na ALLY KIBA huko Nairobi”.

Hatua nyingine TUNDA MAN ameelezea sababu zilizomsukuma kumshirikisha ALLY KIBA katika track ya Msambinungwa “Ally Kiba ni mtu fulani ambaye kiukweli nilikuwa namtamani kufanya nae ngoma muda mrefu sema nilikuwa sijapata ngoma ambayo atafiti vizuri, isitoshe amekaa kimya muda mrefu, kiukweli ile ngoma ameiimba kitofauti sana Ally Kiba alinipa Chalenge sana”.

Post a Comment

 
Top