Menu
 

Msanii Mabeste katika pozi.

Baada ya kuondoka B HITZ MUSIC GROUP Hitmaker wa “Dole” MABESTE kwa sana anafanya zake katika Studio za Uprise Music na mikakati yake ikiwa ni kuubadilisha muziki wa Tanzania, akiwa kama Producer.

“Mimi pia ni Producer lakini sina equipments kwa hiyo Producer Dupy tunashirikiana naye pale kwa sababu yeye anajua kufanya Mastering mimi sijui, na wote tuna idea tofauti kwa hiyo mimi najua kufanya instrumental, nikaona ni mtu mzuri ambaye tunaweza kukaa tukachangiana idea kwa sababu ni producer ambaye yupo flexible anaweza kufanya kazi na mtu yeyote ndani yake kulekule kuna artist LEO MYSTERIO ambaye tulikuwa naye pamoja B HITZ kwa hito tupo pamoja kule” alifunguka kupitia Chumba Cha Sindano katika Kipindi cha Bomba Base Show cha Bomba Fm Radio.

Ameongeza kuwa “Kitu kikumba ambacho sasa hivi kutoka kwangu ni kwamba Mabeste amajiongeza sasa hivi atakuwa anatengeneza nyimbo za tofauti za kuimba na atakuwa anawauzia watu namaanisha kuwa baada ya kutengeneza muziki wangu nitakuwa natengeneza na wa wenzangu pia na maanisha nitaanzisha duka, ambalo tutakuwa tunaunda muziki ambao utakuwa ni package nzima, unajua Producer anatengeneza instrumental anaiuza kwa artist ndio maana artist anasikiliza ile instrumental anafikiria nini cha kuimba, hivyo nitakuwa natengeneza instrumental nampelekea msanii anachagua beat anayohitaji kuisikiliza”.Kwa hatua nyingine MABESTE amezungumzia mikakati yake katika kukuza muziki wa Bongo katika miondoko mingine “Unajua muziki siku zote unabadilishwa na producer, Artist siku zote anatakiwa kusikiliza instrumental halafu anaimba, so kikubwa mimi nina touch zangu ambazo bado zipo kivyanguvyangu hazijawahi kusikika nitaanza kuzitumia niki-release ngoma zangu, kwa hiyo itakuwa Producer MABESTE na mastering DUPY”.

Post a Comment

 
Top