Menu
 


Mzenji anayetamba kwenye kiwanda cha muziki kwa ngoma kama Inatosha, Rudi, Hukumu, Nafsi inauma na sasa Sio sawa SAYNAG ABRIHHAN, ametoa wito kwa wanandoa na wachumba kuvumiliana na kuelimishana pindi suala la ulevi linapomtawala mmoja wao.

Akizungumzia ujumbe halisia uliopo katika wimbo wake wa Sio sawa aliomshirikisha BEKA kupitia kipengele cha Chumba Cha Sindano  katika kipindi cha Bomba Base Show cha Bomba Fm Radio SAYNAG amesema “Sio sawa ni wimbo wa mapenzi, ambayo mwanamke analalamika kutokana na mapenzi na mume wake kwamba akirudi analewa, maneno kila siku na ugomvi hicho ndio sio sawa inazungumzia”.

Amesema lengo kuu la kutoa wimbo huo ni kutoa elimu kwa jamii kutokana na kukithiri kwa vitendo vya ulevi kwa wapendanao hali ambayo husababisha ndoa kuvunjika “Jamii yoyote ambayo wapo walioolewa, wapo ambao hawajaolewa lakini wanaishi wa wake zao namaanisha wanaweza wakaishi na mchumba wake nyumba moja, mtu anaweza akakaa na girlfriend waka nyumba moja halafu mwanaume anaweza akawa na tabia ya ulevi, unajua wanaume wengi wanagumbu eeeh, kuongeaongea sana na kumpigapiga mwanamke”.

Aidha je, SAYNAG anatoa wito gani kwa jamii kupitia wimbo wake wa Sio Sawa “Kama kuna mtu anafanya hizo tabia akisikiliza huwo wimbo anauwezo wa kujirekebisha kwa sababu mimi nimeimba kama mwanamke nafanyiwa hivyo vituko na nalalamika lakini pia BEKA naye ameimba kama yeye ndiye ananifanyia hivyo vituko amekubali kosa na mwisho wa siku akaniomba msamaha”.


Kwa hatua nyingine SAYNAG anasema Jamii inapaswa kujifunza kupitia ujumbe huo ulioimbwa katika ngoma ya Sio Sawa kwa itawawezesha wapendanao kudumu katika misingi ya upendo “Kwa hiyo tunajaribu kuwarekebisha wale ambao wakiona mume wake mlevi akirudi anaongea sana ana tantalila unaona aaaah! ngoja niachane naye labda nitatafuta mwingine hiyo haisaidii kama vipi unaona kwamba mtu wako unampenda inabidi ukae naye, umvumilie na umrekebishe, japo kwamba watu wanasema ukivumilia suala moja unajenga usugu jingine litafuata lakini kama mwanaume anakupenda kwa dhati kujirekebisha ni kitu cha kawaida sana wapo ambao walikuwa walevi sana kweli lakini anapata mwanamke ambaye anakuwa anampenda na anamrekebisha na anaacha tabia alizokuwa nazo mwanzo”.


BOFYA HAPA "LIKE" PAGE YA MWANDISHI WA BLOGU HII

Post a Comment

 
Top