Menu
 

Shetta akiwa na mwanae Qayllah.


Hitmaker wa “Sina Imani” Nurdin Billal a.k.a Shetta amedai kuwa anapokabiliwa na msongo wa mawazo basi mwanae aitwaye Qayllah humfariji sana.

“Maisha mazuri na maisha bado mazuri, Qayllah ni mtoto wangu ambaye nikimuona nafarijika hata kama una stress mbili tatu ukimuona mwanao vile anavyokupandia pandia, unakaa naye una cheka nini unakuwa unasahau vitu vingine ni part of my life, ambayo inanisahaulisha nione kitu kiko sawa tu ni faraja moja wapo” alifunguka kupitia kipindi cha Bomba Base Show cha Bomba Fm Radio kilichopo Mbeya.

Shetta ameongeza kuwa “Unajua wife nini, family vitu vyote kwangu mimi naona kila kitu kiko fresh kiko poa kabisa sijaanza ku-regret maana yake watu wanasema ukiingia katika ndoa kuna vitu vingi nini ila kwangu mimi hakuna vitu vingi”.

Kwa hatua nyingine ameongelea mwenendo wa mwanae baada ya kuulizwa mwanae anaonyesha dalili ya kuwa na kipaji gani? “Qayllah ni mtundu sana bado sijajua kipaji chake huwa naonaona naye ukisikiliza muziki naye anapenda kusikiliza sana, anajaribu ku-dance sana nafikiria fikiria asije kuja kwa baba(yaani kufuata kipaji cha SHETA) (anachekaaaa……..), lakini bado sijajua kipaji chake halisi ni nini ngoja akuekue kwa sababu sasa hivi ana Mwaka mmoja na nusu akifikia miaka miwili au mitatu atajigundua ana kipaji gani”.


Hata hivyo Shetta mwezi huu anatarajia kuachia ngoma mpya yenye ujumbe wa mapenzi akimshirikisha rafiki yake wa karibu Diamond Platinumz, ngoma iliyotengenezwa na Producer Shedy Clever. 

Post a Comment

 
Top