Menu
 


Hitmaker wa Fire Peter Msechu amesema hapendi mwanae Lauren a.k.a Lolo aje kuwa mwanamuziki, bali anataka kumjengea msingi ambao utamfanya aweze kusoma na kupata kazi ambayo itakuwa ikimuungizia kipato cha kudumu.


“Kama mzazi mwanangu namlea katika misingi bora anakula, analala mahala pazuri, na hakikisha baadae anakuja kujitegemea yeye mwenyewe, sitaki ile anakuja kusoma sana halafu halafu baadae afanye muziki hapana” Alifunguka Peter Msechu kupitia kipitia kipindi cha Bomba Base Show ya Bomba Fm Radio, Mbeya.


Kwa hatua nyingine Peter Msechu amezungumzia kuwa kasoro ndogondogo zinazofanyiwa marekebisho ndio sababu moja wapo ya kuchelewa kutoka kwa video ya Fire.“Video ya ngoma ya Fire tuitegemee soon itakuwa inatoka, hivyo kuna marekebisho madogo ilikuwa itoke mapema. Nadhani itakuwa kwenye position ya kutoka ndani ya wiki mbili zijazo kwa sababu kasoro zote tumeshaziweka sawa.” Alisema Msechu.

BOFYA HAPA KUSIKILIZA ZAIDI.

Post a Comment

 
Top