Menu
 


Rapper Bonta kutoka Weusi Entertainment amedai ujumbe mkubwa unaopatikana katika utunzi wa ngoma zake mara nyingi, umekuwa ni changamoto kwake kwa kuonesha uhalisia wa jambo katika video zake na kushindwa kufikisha elimu kwa hadhira.,  

Akifunguka katika kipindi cha Bomba Base Show kupitia Bomba Fm Radio ya Mbeya, Bonta “Ukianza kufuatilia ngoma zangu kuanzia Nauza kura yangu, Matusi, Tukutane Maktaba, Mtaani watu juu, hiyo ndio motion yake idea inakuwa kubwa kuliko hizo video ndio changamoto kubwa inayotukuta especially mimi mwenyewe”.

Kwa hatua nyingine Bonta ameizungumzia ngoma yake mpya ya Laumiwa kuwa inawafungua Watanzania kupigania maendeleo na kukemea tabia za unyonyaji zinazofanywa na viongozi wa siasa au Serikali wasiokuwa wazalendo katika Sekta ya ardhi.

“Mawaziri, wabunge, mahakimu na hata madiwani ni waheshimiwa, lakini Madaktari, askari, waalimu, wanamuziki ni walaumiwa nikiwa namaanisha tumekuwa tukisikia hata barabara ya Kenyatta, Nkuruma, Bibi Titi, Kawawa nk zote hizo ni majina ya wanasiasa, lakini hatujawahi hata kusikia hata kanjia tu labda Ka-Rashid Matumla, au kanjia Ka-Weusi umeona, hiyo sasa ndio dhima ya wimbo huo umeona wanasiasa wamepewa nguvu kwenye mambo yote na kufanya mambo makubwa sana” alisema Bonta.


Post a Comment

 
Top