Menu
 


Rapper Corrine Mary a.k.a Cindy Rulz amedai Kili Music Awards haipo ku-sapport female rappers kutokana na kukosekana kwa kipengele cha Female Rappers of  the year.

Cindy Rulz amefunguka katika kipindi cha Bomba Base Show kupitia Bomba Fm Radio ya jijini Mbeya wakati akelezea mtazamo wake wa tuzo hizo na kudai kuwa hazina maendeleo ya kukuza muziki wa Tanzania bali  zinamanufaa kwa baadhi ya miondoko mingine ya muziki.

“Mfano huwezi ukaniweka category moja na akina Recho au Linnah sijui Dayna itakuwa tofauti, ndio maana ukiona tuzo za watu wa nje huwezi kuona Nick Minaj anapangwa pamoja na watu kama akina Rihanna maybe kama kwenye Videos of the year, lakini kungekuwepo na kipengele cha Female Rappers kipengele ambacho female rappers tunashindanishwa sisi wenyewe kama Chiku Keto, Cindy Rulz, Witness au Stosh, naomba tuzo zetu hazipo katika kusapoti female rappers. Sijawahi kuona yaani Female Rappers wasanii wazamani kama akina Zay B, Sister P na Rah P wakitunzwa na hizi tuzo kutokana na kukosa hicho kipengele” alisema Cindy Rulz.

Ameongeza kuwa utaratibu wa kuachia ngoma zake mpya huwa ni tofauti na wasanii wengine kutokana na wengi wao ku-target kipindi cha utoaji wa tuzo “Well to be honest Sijawahi kufanya kazi zangu za muziki nikaweka nguvu sana kwamba nafanya hii ngoma ili itue kwenye Kili Music Awards hapana, nakuwa natengeneza muziki mzuri kwaajili ya kuwafurahisha mashabiki, ukiwa unatengeneza muziki kwaajili ya tuzo aaaah, hiyo dizaini inakuwa kazi sana kwa sababu incase imetokea bahati mbaya hujawa nominated unaweza ukadata, mimi natengeneza muziki mzuri na tuzo iwe tu kama bonus, yeah kama jina lilivyo nitunzwe tu kwa sababu nafanya kitu kizuri “.Hata hivyo ameeleza lengo lake kuu kwa sasa nikuhakikisha nyimbo zake zinafikia katika soko la kimataifa na si tuzo, “Nipate tuzo nisipate tuzo bado nitaendelea ku-push muziki wangu sehemu ambayo kwangu ningependa uweze kufika, kama ikitokea bahati nzuri nimekuwa nominated na nikashinda yote heri, lakini focus yangu haipo hapo focus yangu nikutengeneza muziki mzuri hits song after hits song, good music watu waupende tuendelee kusonga na maisha kama vitu vingine”.

Post a Comment

 
Top