Menu
 

Kiungo kutoka nchini Hispania, Thiago Alcantara ametupa dogo kwenye klabu ya Barcelona kwa kusema klabu hiyo haikuonyesha kumuamini wakati alipo pandishwa kwenye kikosi cha kwanza tangu mwaka 2009.


Thiago Alcantara amesema anaamini hali hiyo ilikua ni kichocheo kikubwa kwa viongozi wa klabu ya Barcelona kufikiria kumuuza mwanzoni mwa msimu huu, hali ambayo ilifanikiwa baada ya uongozi wa FC Bayern Munich kuwasilisfa ofa ya kutaka kumsajili.


Alcantara amesema wakati akiwa Camp Nou aliamini huenda angekua gwiji wa soka wa klabu ya Barcelona kutokana na uwezo mkubwa alionao, lakini mawazo hayo hayakuwepo kwa viongozi wake na mwishowe walishindwa kuuthamini mchango wake.


Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 22, amesema kwa sasa anajihisi ni mwenye furaha akiwa na klabu ya Bayern Munich tena chini ya meneja ambae alikilea na kukikuza kipaji chake Pep Guardiola.


Hata hivyo Thiago Alcantara amesisitiza kwamba aliposikia yupo kwenye mpango wa kuondoka katika klabu ya Barcelona hakusita kufanya hivyo kwani aliamini umri alio nao ni mdogo na alikua na nafasi nyingine ya kuthibitisha yeye ana ubora gani anapokua uwanjani.


Kutokana na kiwango kizuri anachokionyesha akiwa na klabu ya Bayern Munich ya nchini Ujerumani, Thiago Alcantara alitajwa kwenye kikosi cha timu ya taifa ya nchini Hispania ambacho hii leo kinacheza mchezo wa kimataifa wa kirafiki dhidi ya timu ya taifa ya Italia.

Tangu aliposajiliwa na klabu ya Bayern Munich Thiago Alcantara tayari ameshaichezea klabu hiyo katika michezo 12 na kufanikiwa kufunga mabao mawili.

Post a Comment

 
Top