Menu
 

Hitmaker wa Jambo Jambo Steven William a.k.a Steve wa RnB anatarajia kutangaza ndoa na mpenzi wake aliyemvija pete mwenzi Novemba mwaka jana, mara baada ya kumaliza ziara yake nchini Marekani.

“Ni kweli tunapendana, soon soon nitatangaza ndoa, baada ya safari yangu ya Marekani mwezi huu Machi nahisi itakuwa mapema tu baada ya kutoka huko” alisikika Steve wa RnB akifunguka kupitia kipindi cha Bomba Base Show  kupitia Bomba Fm Radio iliyopo jijini Mbeya.

Ameongeza daima ataendelea kufanya RnB, kwani ndio imemfanya Steve wa RnB kufahamika na kujitofautisha na wasanii wengine, na kuendelea kuwadhihirishia fans wake kuna project inakuja kama albamu na ina nyimbo nyingi ambazo amewashirikisha  wasanii wa Nje na ndani ya Bongo.


“RnB ni kitu nachokipenda najisikia niko comfortable, napofanya na enjoy na kuburudika any time ndio maana huwa nafanya kitu ambacho mashabiki wanakipenda kwa hiyo hata wimbo unapofika kwa mashabiki unakuwa wa aina yake nakuonekana mimi watofauti sipendi kufanya kama watu wengine wanavyofanya kwa kukimbilia kuimba afro pop” alisema Steve wa RnB.

Post a Comment

 
Top