Menu
 


Shirikisho la soka nchini TFF limetoa sababu za kushindwa kuitafutia michezo ya kimataifa ya kirafiki timu ya taifa ya Tanzania dhidi ya timu kubwa duniani kama inavyokua kwa mataifa mengine barani Afrika kama Afrika kusini ama Ghana ambazo mara kadhaa zimekua zikicheza na timu za rtaifa kutoka barani Ulaya ama Amerika ya kaskazini na kusini.

Afisa habari na mawasiliano wa TFF Boniface Wambura amesema wanapenda kuiona timu ya taifa ya Tanzania ikicheza michezo ya kirafiki na mataifa makubwa duniani lakini kinachowapa changamoto ni gharama za maandalizi ya michezo hiyo kuwa kubwa.


Shirikisho la soka nchini TFF limelazimika kutoa sababu hizo, kutokana na wadau wa soka nchini kuiona timu yao ya taifa ikicheza na mataifa ya kawaida tena ya barani Afrika, kitu ambacho kinadhaniwa hakiisaidii Taifa Stars kupanda katika viwango vya ubora wa soka duniani, ambavyo hutolewa kila mwezi na shirikisho la soka duniani FIFA.

Wakati huo huo timu ya taifa ya Tanzania imecheza mchezo wa kimataifa wa kirafiki dhidi ya timu ya taifa ya Namibia huko mjini Windhoek.


Matokeo ya mchezo huo ni kwamba Taifa Stars 1 na Namibia 1.

Post a Comment

 
Top