Menu
 

Msanii wa muziki wa kizazi kipya Tanzania TOP C katika pozi


Hitmaker wa Lofa TOP C amedai kutopokea simu kwa Menenjimenti yake ya Candy n Candy Records ya nchini Kenya ndio sababu kuu inayomfanya kushindwa kujua hatima yake ya kuvunja mkataba kwa madai aliyotoa Februari 5, mwaka huu kuwa menejimenti yake imejaa ubabaishaji.

Akifunguka karika Kipindi cha Bomba Base Show kupitia Bomba Fm Radio cha Jijini Mbeya, Top C ambaye ilitakiwa avunje mkataba wake na Candy n Candy Records Februari 12, alisema “ licha ya kutumia mbinu mbalimbali za kuonana nao ili kuvunja mkataba zinagonga mwamba, nawaomba Watanzania wenzangu waniombee niweze kufanikisha kuumaliza mapema na kuwa huru, kutokana na huu mtihani ujajua.

“Nipo kwenye wakati mgumu hawapokea simu, lakini lazima nikae na kamati yangu ili kuandika uamuzi wangu wa mwisho na kamati yangu nao waweze kuzungumza nao uamuzi wao wa mwisho kama Candy n Candy Records hawataendelea kupokea simu” aliongeza Top C.

Sababu kuu zinazomfanya Top C kuvunja mkataba na Candy n Candy Record ni pamoja na “Mikakati yetu na ile kampuni bado haijakuwa katika mstari ambao unaeleweka kuna vitu vingi  sana ambavyo kampuni imeahidi lakini bado havijaanza kutendeka kazi unaonena vile kama kuna ubabaishaji mwingi, mkataba unasema kuwa kuna muda wa kufanya promotion na muda fulani mtakuwa mmefanya nyimbo kadhaa”.

Post a Comment

 
Top