Menu
 

Mahakama ya Wilaya ya Mbarali Mkoani Mbeya imemwachia huru Mwalimu Andrew Shadrack aliyekuwa anakabiliwa na tuhuma za kuwabaka wanafunzi watatu wa Shule ya Sekondari ya Mont Fort Septemba 12, 2014 majira ya saa tatu usiku hadi saa tano usiku.

Kesi hiyo ilifikishwa Mahakamani hapo na Mwedesha mashitaka Mazoyea Luchagula mbele ya Hakimu wa Wilaya Kinabo Minja ambapo ilidaiwa kuwa kosa hilo ni kinyume cha sheria namba 130 na 131 sura ya 16 iliyofanyiwa mapitio mwaka 2002 na mshitakiwa alikana kutenda kosa.

Upande wa mashitaka ulileta mashahidi tisa watatu wakiwa ni wahanga wa tukio hilo,Matroni,Daktari,Askari mpelelezi na Kielelezo cha vipimo vya Polisi(PF 3) ambavyo vyote vilishindwa kuthibitisha kumtia mtuhumiwa hatiani.

Akisoma hukumu hiyo Hakimu amesema pamoja na vipimo vya Daktari kuonesha majeraha sehemu za siri kwa wahanga lakini havikuonesha kuingiliwa kimwili kwa wanafunzi hao pia wenyewe kuwa na maelezo yanayofanana,pia kushindwa kutoa taarifa kwa uongozi wote wakidai walikuwa na hasira kwa kitendo walichotendewa na Mwalimu wao.

Aidha Kinabo amesema kuwa PF 3 ilikuwa na mapungufu kwani mbili zilionesha watoto watoto kupimwa Septemba 13 na mmoja kupimwa Septemba 14 hali inayotia shaka ushahidi huo wakat tukio lilitokea siku moja na PF 3 hizo kutolewa katika vituo viwili vya Polisi vya Rujewa na Mbarali.

Ameongeza kuwa PF 3hizo zilikuwa na miandiko ya wino tofauti hali ambayo Kinabo ametilia shaka pia akisema kuwa mshitakiwa baada ya kukamatwa alipelekwa Polisi na wahanga kuachwa Bwenini ambapo walienda kutoa taarifa na maelezo siku iliyofuata.

Kutokana na ushahidi kushindwa kumtia hatiani mtuhumiwa Mahakama imemwachia huru baada ya kukosekana ushahidi usio shaka,ambapo Kinabo amesema kuwa upande ambao haujaridhika unaeza kukata Rufaa kwa kipindi kisichozidi siku thelathini.

Mwendesha mashitaka alikuwa akihaha kuaandaa taratibu za kukata Rufaa kutokana kutoridhika na hukumu iliyotolewa na Mahakama hiyo ya wila ya Mbarali.

Wakati huo huo watumishi watano wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali wamefikishwa kizimbani kwa makosa ya kuhujumu uchumi na kuisababishia hasara Halmashauri hiyo.

Mwendesha Mashitaka wa TAKUKURU Nimrod Mafwere amewataja washitakiwa hao kuwa ni pamoja na Mganga Mkuu wa Wilaya ya Mbarali Somoka Mwakapala,Francis Kapinga Mhasibu,Lazaro Mgimba ambaye ni mhasibu msaidizi,Venance Mwashala na Alfred Mbewa.

Kwa pamoja imedaiwa Mahakamani hapo kuwa watumishi hao kwa kutumia nyadhifa zao wamwibia mwajiri wao jumla ya shilingi 3,400,000/- kwa madai ya kuendesha mafunzo ya TB na ukimwi kwa watumishi na Mafunzo mengine Mkoani Morogoro.

Kwa kutumia madaraka yao walitoa Benki kiasi hicho cha fedha kwa kumtumia mwanafunzi wa chuo cha uganga aitwaye Allen Charles Januari 8 na 9 mwaka 2009 ambapo fedha zilitolewa Benki siku hiyo zikiwa katika mchangano wa shilingi 3,030.000/- kama fedha za mafunzo na shilingi 270,000/- kama posho kwa watumishi watatu ambao saini zao ziligushiwa na watuhumiwa hao.

Kwa upande wa mashitaka taleta mashahidi 10 na vielelezo 20 katika kesi ya kwanza, kesi ya pili mashahidi11 na vielelezo 16 na kesi imeanza kusikilizwa ambapo shahidi wa kwanza ambaye ni Afisa wa TAKUKURU Mbarali Halfan Abdala ameanza kutoa ushahidi.

Kesi imeahirishwa hadi tarehe 11 June mwaka huu itakapoendelea kusikilizwa.

Post a Comment

 
Top