
Utoaji wa tuzo za BET 2014 unaendelea usiku huu na tayari
Davido toka Nigeria ametangazwa kuwa mshindi wa tuzo ya Best African
Act.
Kipengele hicho kilikuwa kinawaniwa na mshindi huyo pamoja na wasanii
wengine wakubwa Afrika ambao ni Diamond Platinumz, Mafikizolo, Toofan,
Sarkodie na Tiwa Savage.
Tuzo hiyo imetolewa muda mchache kabla ya kuanza kwa show kubwa ya
utoaji wa tuzo hizo inayopambwa na burudani kutoka kwa Drake, Nicki
Minaj, Usher Raymond na wengine wengi.
Diamond Platinumz ambaye ameiwakilisha vizuri Tanzania licha kutopata
tuzo hiyo, ameandika ujumbe wa kiushindani katika Instagram unaoonesha
ukuaji katika game la kimataifa.

“Tusipopenda kukubali Matokeo na Ushindi wa Wenzetu basi Daima
Hatutaweza kuwa Washindani....Muhimu ni kujua wapi tulipotoka na Wapi
tulipo Leo... Katika Nchi zaidi ya 20 zenye wasanii zaidi ya Million 40,
kuchaguliwa Tanzania ni fursa, Heshima na Hatua kubwa... Cha Muhimu ni
kuitumia vyema Fursa Hii na Kuhakikisha Mwakani tunapiga Hatua
Zaidi!.... Asante sana kwa wote wanaozidi kuni support kwa hali na Mali,
Mapambano ndio kwaaaanza yanaanza sasa.....!!!!!! @wcb_wasafi For Life
Baby.”
Ni kweli Diamond amepiga hatua kubwa sana na hata kuifanya Tanzania iwe miongoni mwa nchi zilizotajwa katika tuzo hizo kubwa.
Credits:- Times Fm
Post a Comment
Post a Comment