Menu
 

Hitmaker wa Naumia Roho DULLAYO amekiri nyimbo zake kadhaa kumwendea mrama ikiwemo ngoma ya Watu wabaya aliyofanyia katika Studio za Tongwe Records hali iliyomfanya kurejea kufanya style zake za awali.

Akichanika kupitia Bomba Base Show ya Radio Bomba FM, DULLAYO amesema alianza kuhisi mapema  kuwa ngoma yake hatopokelewa vizuri kutokana na kuimba kimasihala.'' Sikujipanga na sikuwa serious kihivyo nilikuwa na matatizo kidogo so nilikuwa nasikuisambaza katika Media nyingi na wakati mwingine nilikuwa naulizwa kama nimeachia official lakini nilikuwa sina majibu, lakini pia nimepata somo nataka kurejesha style zangu za zamani kama Naumia roho, Twende na mimi au Mida ya kazi''.

DULLAYO amesema kwa kudhihirisha kuwa style zake za awali ndizo zilizokuwa zikimfanya kuheshimika katika Music Industry nakukonga nyoyo za mashabiki mwezi huu ataachia ngoma yake ya kwanza inayokwenda kwa jina la Mdebwedo aliyomshirikisha msanii kutoka kongo KENNEDO.

''Kwa sababu ya matarajio yangu kutofikia mafanikio, kwa hiyo hivi soon nitaachia Video pamoja na audio ikiwa katika miondoko ya Rap, nitaachia mwezi huu inafanana na miondoko ya Naumia Roho so fans wangu wakae mkao wa kumeza kwani watamsikia DULLAYO yuleyule wa kwao wakipindi cha nyuma''.

Kwa upande mwingine DULLAYO kama mzazi amemwelezea Mtoto wake SAMEEL kuwa huenda akaja kuwa mtu maarufu sana kutokana na dalili anazozionesha kupitia vitu anavyovipenda na anampa baraka zote za mafanikio.

''Mimi na mtoto mmoja anaitwa SAMEEL ana umri wa mwaka mmoja, lakini bado sijaoa ila mtoto wangu namlea vizuri, mimi nafikiri mtoto wangu atakuwa star jinsi navyoona utundu wake nini licha ya kuwa anaumri mdogo lakini anapenda sana muziki, japo sipendi mwanangu ajekuwa mwanamuziki napenda asome awe msomi na elimu imkomboe na kuwa msaada mkubwa katika jamii na taifa kwa ujumla''.

Post a Comment

 
Top