Menu
 

Shughuli za uchimbaji wa madini husaidia sana katika kukuuza uchumi wa nchi zinazoendelea kama Tanzania, lakini shughuli hizi za uchimbaji huathri mazingira na athari yake kuonekana kwa vizazi hadi vizazi. Hii ni kwa mujibu wa Science Direct Tanzania.

Sheria ya usimamizi wa mazingira ya mwaka, 2004 kwa sekta ya madni na kanuni ile ya ziada ya mwaka 1999 yote kwa pamoja zinazitaka sekta za madini kusimamia na kulinda mazingira katika shughuli zao za uchimbaji.

Athari za kimazingira zinazoweza kuhisiwa kwa sababu ya uchimbaji wa madini ni pamoja na mmomonyoko wa udongo, uchafuzi wa udongo chini ya maji, uchafuzi wa maji unaotokana na kemikali kama arseniki, sufuriki na zebaki zinazotumika katika shughuli hiyo huathiri afya ya binadamu, huaribu ubongo, ini, nywele kunyofoka, mgozi kugeuka na ukuaji wa mtoto huathirika. Ni kwa kiasi gani sheria hii inafuatwa na makampuni ya migodi yanayochimba madini? Na, ni athari zipi zimeshakwisha tokea kwa sababu ya sheria hii kutokuzingatiwa?

 Kwa wale waliokosa kipindi chetu cha wiki iliyopita kilichokuwa kinahusu athari za kiafya zinazowakuta wananchi kutokana na shughuli za uchimbaji wa madini

http://youtu.be/FkCc31jJXec

Post a Comment

 
Top