Menu
 

 Mchungaji Daniel Mwasumbi aachiwa huru

Mahakama Kuu Kanda ya Mbeya, imebatilisha hukumu  ya kifungo cha miaka 30 jela na viboko 12 aliyokuwa akiitumikia Mchungaji wa Kanisa la EAGT la Iwambi Jijini Mbeya,  Daniel Mwasumbi(57) aliyekuwa akikabiliwa na kesi ya ubakaji na kumpa mimba mwanafunzi wa Shule ya Sekondari Itende Neema Beni(19) jijini hapa.
 
Mchungaji Mwasumbi alihukumiwa kifungo hicho, Januari 2 mwaka huu na mahakama ya Wilaya ya Mbeya na Hakimu Gilbert Ndeuruo na Serikali kuwakilishwa na wakili Achiles Mulisa, ambapo Mahakama ilimtia hatiani Mchungaji katika makosa kinyume cha sheria kifungu cha 130(2)e na 131(1) sura ya 16 ya sheria iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2002.

Awali Mchungaji Mwasumbi alikuwa akitetewa na Wakili wa kujitegemea Victor Mkumbe ambapo ilidaiwa kutenda makosa hayo kati ya Januari 2008 hadi 2011 ambapo alimpa ujauzito na kumzalisha mwanafunzi huyo watoto wawili wa kiume kwa nyakati tofauti hivyo kumkatisha masomo kinyume cha sheria.

Katika Rufaa hiyo Mchungaji  Mwasumbi alikuwa akitetewa na Wakili wakujitegemea Benjamin Mwakagamba kutoka Dar es Salaam wakati Serikali iliwakilishwa na Wakili Prosister Paul.
 
Akisoma hukumu ya rufaa hiyo, Jaji wa Mahakama Kuu Kanda ya Mbeya, Atuganile Ngwala,  alisema kuwa sababu zilizowasilishwa kwenye mahakama  hiyo na Wakili wa upande wa utetezi zilidhihirisha kuwa kulikuwa na ukiukwaji wa kisheria kwenye hukumu hiyo.
 
Jaji Ngwala ambaye alitumia takribani saa 1:15 kusoma huku hiyo alisema katika utoaji wa hukumu hiyo haukuzingatia vipengele muhimu vya kisheria viilivyotumika na mahakama ya wilaya kumtia hatiani Mchungaji Mwasumbi.
 
“katika rufaa hii ni kweli kuna mambo mengi ambayo yanaonekana kukiukwa katika utoaji wa hukumu, kama zilizovyoweza kuanishwa na wakili wa utetezi hivyo na mimi nakubaliana na wakili Mwakagamba (wakili wa utetezi) kwamba kulikuwa na ukiukwaji wa kisheria kwenye hukumu hiyo” alisema
 
Aliongeza kwamba kama ilivyoelezwa na wakili Mwakagamba,  muda wa lilitopotekea tukio hilo na liliporitiwa kwenye vyombo vya usalama unaonekana kuchelewa na kukinzana,  lakini pia ushahidi ulitolewa mahakamani hapo na Mhanga  ulionekana kujichanganya hivyo haujaonesha mrufani kutenda kosa hilo’.
 
Awali Jaji Ngwala alimwita mchungaji Mwasumbi kuwa ni mende, na ni mtu hatari sana katika jamii kwa kosa kama hilo na hafai kuwa katika jamii jambo lililowafanya watu waliokuwa wakifuatilia mwenendo wa hukumu hiyo kuanza kuinamisha vichwa chini akiwemo Katibu wa Kanisa la Uinjisti Bwana Mwakasole.
 
Lakini  baadaye, Jaji Ngwala alionesha hisia zake kwamba kutokana na kujichanganya kwa ushihidi hususani wa shahidi namba moja ambaye ni binti aliyefanyiwa kitendo hicho hivyo kumtoa hivyo na haonekani kama ana kosa.
 
Alisema ‘Nasema hivi mtu huyu alikuwa ni mende na ni hatari sana katika jamii asiyefaa kwa namna yoyote ile na anastahili adhabu kali laiti kama ingethibitika hivyo, lakini hapa ushahidi umeshindwa kuthibitisha hili hivyo ana haki ya kuachiwa huru’.
 
Hata hivyo, Jaji Ngwala alisema kuwa kwa upande wa Jamhuri ambao ulikuwa ukiongozwa na wakili wa Serikali, Prosister Paul una haki zote za kukata rufaa na kesi kuanza upya endapo utaona haujaridhika na hukumu hiyo.
 
Wakili aliyekuwa akimtetea Mchungaji Mwasumbi alisema kuwa katika rufaa ya mteja wake aliwasilisha sababu saba za kupinga hukumu hiyo ambapo alidai kuwa  hakimu wakati wa kutoa hukumu hiyo alikosea kisheria na haki muda wa kuripotiwa kwa shauri hilo kwa vyombo vya usalama na lilipotokea ulikinzana na kwamba aliegemea kwa ushahidi wa Mhanga tu.
 
Sababu zingine alidai kuwa hakimu aliegemea katika ushahidi  au vidhibiti ambavyo awali alivikata mwenyewe, pia alidai kuwa hakimu hakuangalia uhalisia kosa lenyewe na badala yake alionekana kutoa maoni yake binafsi.
 
Lakini sababu nyingine wakili Mwakagamba alisema kuwa hakimu huyo, aliegemea ushahidi ambao ulijichanganya, wendesha mashtaka  walishindwa kuwapeleka mahakamani hapo  mashahidi wa msingi katika kesi hiyo, hakimu aliegemea upande wa vyeti vya watoto wawil waliodaiwa ni wa Mchungaji Mwasumbi ambapo vyeti vilidurufiwa (photocopy) na si vyeti halisi na  mwisho hakimu huyo alitoa hukumu ambayo haikufuata mtiririko uliosahihi wa mashahidi husika.
 
Akizungumza na gazeti hili, mtoto wa Mchungaji Mwasumbi,  Elizabeth Mwasumbi alisema anamshukuru Mola kwa kumwezesha Jaji Ngwala kwa kutenda haki katika rufaa ya baba yake.
 
Alisema; ’Mimi na wenzangu tulikuwa na wakati mgumu sana pindi baba yetu akiwa ndani, kwani mimi niliathirika sana kiafya na kiuchumi nilishindwa kufanya shughuli yoyote kutokana na mawazo lakini namshukumuru Mola kwa kutenda haki’.

Hata hivyo nje ya Mahakama ndugu na jamaa waliofurika kusikiliza hatma ya Rufaa hiyo waliokuwa na hamu ya kumlaki kwa furaha Mchungaji Mwasimbi ambaye pia ni mwimbaji wa nyimbo za Injili kushindwa kutokana na Maafisa wa Magereza kumpeleka Gerza la Ruanda kukamilisha taratibu za Magereza.


Post a Comment

 
Top