Menu
 

Mshindi wa Redds Miss Mbeya 2014 Atukuzwe Fabian  akiwa na washindi wengine Anitha Patrick msindi wa pili(kushoto) na Huku Matrida Hilu  msindi wa tatu(kulia),  baada ya kupatikana msindi katika shindano hilo lililofanyika jana City Pub jijini Mbeya ambapo Waratibu na waandaaji ni Bomba FM Radio kupitia BOMBA ENTERTAINMENT
Redds Miss Mbeya 2014 Atukuzwe Fabian akikabidhiwa zawadi yake na Balozi wa Access Computer Limited ambao ni miongoni mwa wadhamini wa shindano hilo


Wazee wa Ngwasuma kama kawaida yao
Timu ya majaji kabla ya kumtangaza mshindi.


Na Emanuel Madafa, Mbeya
Kinyanganyiro cha kumtafuta mnyange wa mkoa wa Mbeya kwa mwaka 2014, kiliteguliwa usiku wa ijumaa baada ya Mrembo Atukuzwe Fabian  msomi wa chuo kikuu kwa  kuwabwaga warembo wengine 11 waliojitokeza katika Kinyang'anyiro cha Redds Miss Mbeya.
Shindano hilo lililofana na kukonga nyoyo za mashabiki waliohudhuria, kutokana na washindi hao kupatikana kihalali liliratibiwa na kituo cha redio BOMBA FM cha mkoani Mbeya kupitia kitengo cha BOMBA ENTERTAINMENT.

Nyota ya mrembo huyo ilianza kuonekana mapema, katika mavazi yote aliyovaa, lakini zaidi aliwapagawisha mashabiki wa urembo waliofurika katika ukumbi wa City Pub  baada ya kujibu swali kwa ustadi lililouliza atamshauri nini Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Abaas Kandoro endapo atapata fursa ya kukutana naye.

Mshindi wa Pili katika shindano hilo   ni Anitha Patrick Huku Matrida Hilu akishika nafasi ya Tatu .

Washindi hao watawakilisha mkoa wa Mbeya  katika shindano la kanda mwishoni mwa mwezi huu Mkoani Iringa .

Hata hivyo katika mtanange huo Bendi Maarufu na Kongwe katika Nyanja za burudani toka jijini Dar es salaam Fm Academia wazee wa ngwasuma wakiongozwa na Nyoshi,Patcho Mwamba na Baroteli waliweza kuwapagawisha mashabiki na wapenda burudani walifurika katika viwanja hivyo vya City Pub jijini Mbeya.

Pamoja na Burudani hiyo pia wapenzi wa burudani waliohudhuria katika viwanja hivyo vya city Pub wamedai kuwa shindano hilo limekuwa la kipekee hasa kutokana na kuwepo kjwa ulinzi wa kutosha pamoja na hali ya hewa kuwa nzuri tofauti na mwaka jana.

Post a Comment

 
Top